Wednesday, March 4, 2015

HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA YAZIDUA UPIMAJI, USIKIVU WA WATOTO WACHANGA.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman amesema sikio, mdomo na macho ni sehemu muhimu sana katika maisha ya binaadamu hivyo unapokuwa na wataalamu wa kushughulikia viungo hivyo ni neema kubwa inayopaswa kuenziwa.

Haya ameyasema katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga mara baadaya kuzaliwa ili kujua matatizo yao.
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga.

Amesema uchunguzi wa watoto wachanga kujua usikivu wao mapema ni mpango mzuri ambao utalisaidia Taifa kuwa na watoto wenye usikivu mzuri na njia rahisi ya kuwapatia matibabu kwa watakaogundulika na matatizo hayo.

“Kujua tatizo la kiafya mapema na kuanza kulishughulikia kunapunguza gharama za matibabu hivyo nawanasihi wazazi kuwapeleka watoto wenu mara baada ya kujifungua, ”alisisitiza Waziri wa Afya.

Wafanyakazi wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.

Amesema maradhi ya usikivu yamekuwa yakiwasumbua watoto wengi Zanzibar na iwapo kila mzazi atatimiza wajibu wake wa kumpeleka mtoto wake kupata vipimo yataweza kupungua.


Waziri wa Afya aliwataka wazazi kuwa na utamaduni wa kuzalia Hospitali ili kupata huduma hiyo kwa urahisi na watakaozalia majumbani kuwapeleka watoto wao kuchunguzwa usikivu mara baada ya kuzaa.

Daktari Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Aidha Waziri huyo aliwataka madaktari waliopatiwa mafunzo ya kutoa huduma hiyo kuwa waadilifu katika kutekeleza kazi zao kwani huduma za watoto wachanga na wazazi zinahitaji uvumilivu.
Waziri alisema tatizo la uskivu huazia mtoto anapochelewa kulia mara baada ya kuzaliwa ama wanapopata homa ya manjano, kutopatiwa chanjo, mzazi kuchelewa kuzaa baada ya uchungu wa muda mrefu na kuzaliwa mtoto bila ya ya kufika muda wa kuzaliwa.

Mjumbe wa Bodi ya ZOP Yahya Mohammed Slim akitoa maelezo kuhusu Jumuiya hiyo inavyotoa huduma za kijamii vijijini katika usinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Nao madaktari walio patiwa mafuzo hayo walisema kuwa wana uwezo mzuri wa kuwapima usikivu watoto na kubaini matatizo yao na kuishauri Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia watoto watakaozaliwa vijijini.


Mradi huo wa kupima watoto usikivu ulipokea msada wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kutoka Jumuiya ya Madaktari wanotoa huduma za matibabu vijijini ( ZOP) ambavyo vina thamani vya Dola elfu 50 za kimarekani.

Iran:Marekani yapinga msimamo wa Israel


Rais Barrack Obama wa Marekani na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyah.

Rais Obama amepuuzilia mbali onyo alilotoa waziri mkuu wa Israel kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear katika hotuba yake tata kwa bunge la Marekani.

Bwana Obama amesema Benjamin Netanyahu alishindwa kutoa suluhisho mbadala kuhusu suala kuu la jinsi ya kuizuia Teheran kutengeza silaha za Nuclear.

Bwana Netanyahu ambaye alialikwa kuhutubia bunge na viongozi wa chama cha Republican alishutumu mkataba uliowekwa kati ya mataifa ya magharibi na Iran na kudai kuwa ni hatari .

Iran imesema kuwa hotuba hiyo ilikuwa ikiudhi na ni ya kujirudia.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, anatakiwa kusafiri Saudi Arabia leo Jumatano kuhakikishia mataifa ya ghuba kuwa mkataba huo utaimarisha nafasi ya Iran katika eneo hilo.