Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akisisitiza jambo juu ya Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni Uislamwa Huruma. |
TAARIFA KWA
UMMA WA KIISLAM
Sikuambii
Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa Waumini wa Kiislam mpaka akafikia mahala
akasema “Yoyote mwenye kukiri Mungu ni Mmoja, mtu huyo ataingia peponi”hii ndio
huruma ya Mtume (s.a.w.w) na Uislam aliotuletea.
Sasa
ndugu yangu wewe unapata wapi fatua, unapata wapi Rai, unapata wapi Aya na
Hadith za kumuambia mwenzako huyo ni Mtu wa Motoni wakati anasema Lailaha
ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah) Fatwa hiyo umeipata wapi?
Ni
kwa mantiki gani unaetoa fatua ya kuuwawa Yule ambae unaetofautiana nae na yeye
anasema Lailaha ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah) Fatwa hiyo
umeipata wapi?
Unapata
ujasiri upi wa kuchukua mkono wako ukamuua mtu anaesema Lailaha ilallah (Hakuna
Mola apasaekuabudiwa ila Allah)ujasiri
huo umeupata wapi?
Unatoa
kwenye Qur’an gani fatua ya kuvaa bomo kwenda kulipua ndani ya Msikiti watu
wanaosema Lailaha ilallah (Hakuna Mola apasaekuabudiwa ila Allah) Fatwa hiyo
umeipata wapi?
Uislam
wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bado haujulikani, Mnayo kazi ya kuwaeleza watu
Uislam wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni Uislam wa Huruma.
Imetolewa na
Kiongozi
Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh
Hemed Jalala.
Ijumaa,
02-12-2016.