Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Mh. Raymondi Mushi ametoa wito kwa kila mwananchi kuhifadhi na kutunza vyanzo
vya maji pamoja na kupanda miti kwa maeneo anayoishi.
Amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa
habari katika Uzinduzi wa kuadhimisha siku ya mazingira Duniani ,Dar es salaam
na kuwahimiza Wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kufanya usafi katika
maeneo yote ya makazi na biashara.
Aidha Mushi amewatahadharisha wakazi na wananchi
wote amabao ni wachafunzi wa mazingira kuacha mara moja kwani atakayekiuka
taratibu za usafi na kusababisha uchafuzi wa mazingira atachukuliwa hatua za
kisheria.
Mh Mushi amewahimiza Wakandarasi wanaotoa huduma ya
uzoaji taka katika wilaya ya Ilala kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kutosha na
kutoa huduma inayokidhi mahitaji kwa wananchi.
Hatahivyo Mh Mushi ametoa wito kwa kila mkazi wa
Halmashauri ya Ilala kushiriki kikamilifu kwa pamoja katika wiki hii hadi
tarehe 5 ambapo ni kilele cha kuadhimisha siku ya mazingira Duniani.