Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh
Hemed Jalala ameitaka Watanzania waweze Kujuana, ili Watanzania waweze kukaa
kwa Amani, Kusaidiana na kukaa mahala pamoja.
“Ndugu zangu Viongozi, Watu wasiotambuana ni Vigumu
kuelewana, Watu wasiotambuana ni Vigumu kusaidiana, Watu wasiotambuana ni
Vigumu kukaa mahala pamoja, hivyo malengo makubwa kwa kweli ya Kikao hiki na
Mwito huu, ni Kutambuana” Alisisitiza Sheikh Jalala
Sheikh Jalala alitoa wito huo wakati akiongea Katika Kikao
cha Pamoja na Viongozi wa Kata ya Kigogo kilichofanyika Jana Masjid Ghadir,
Kigogo Post Dar es salaam, kikiwa na lengo kuu la Kutambuana, ambapo walihuria
Wajumbe wa Mashina, Wenyeviti na Makatibu wa Serikali za Mitaa, Maafisa
Watendaji wa Mitaa, Polisi wa Kata, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata.
Aidha Sheikh Jalala pia amewataka Watanzania Waislamu,
Wakristo pamoja na Wapagani kuwa na Mapenzi ya Kupenda nchi yako, Mahali ulipo
zaliwa kwa kufanya hivyo hutoweza kusababisha upotevu wa Utulivu na Amani
pamoja na huduma mbovu kuwepo katika mji wako.
“Jambo la kupenda nchi yako, tunapozungumza habari hii ya
kupenda nchi yako baadhi ya watu wasioelewa huwa hawatambui kupenda nchi yako,
lakini kupenda mahali unapoishi, kupenda mahali ulipozaliwa na kupenda nchi yako
maana yake ni nini? Maana yake ni kutaka make vizuri katika mji huo, ni kutaka
utulivu uwepo katika mji huo,ni kutaka uchumi mzuri uwepo katika mji huo, ni
kutaka maradhi yasambaratike katika mji huo,ni kutaka Ujinga usambaratike
katika mji huo, ni kutaka Watu wawe na afya nzuri katika mji huo,Viongozi sisi
tunaamini ya kwamba Uislamu tunaoamnini sisi ni Uislamu wa kuipenda nchi yako,
wakupenda taifa lako, na ya kupenda Kigogo yako.” Alisema Sheikh Jalala
Kwa Uapnde wake Mkuu wa Kituo cha Kigogo Post Ndugu Alex Duguza ameishukuru Jumuiya ya
Waislamu T.I.C na kuitaka iendelee na kuisadia Jamii ya Kigogo na Watanzania
kwa Ujumla pamoja na kuwataka Viongozi kuwalea watoto katika mafunzo ya Dini.
“Mimi niombe Msikiti huu au Jumuiya hii kwa Ujumula waendelee
kusaidia, Kigogo ni yakwetu sote, tuliopo Kigogo hatakama hatuishi Kigogo,
tukishafanyia kazi kigogo tayari ni kwetu, sisi ndio tutaifanya Kigogo iwe
salama” alisema Duguza
“Viongozi niuwatake tuwatake watoto wetu wafuate maadili ya
Dini zetu, tunaposema maadili ya dini zetu hatumaanishi kwamba kila mtu awe ni
Shia Ithnasheriya Sheikh Jalala ameeleza Vizuri,hakuna dini inayosema nenda
ukaue, hakuna dini inayosema mdharau baba yako, Kila Dini inahubiri Upendo,
Amani, kuheshimiana, tuwaeleze jamii inayotuzunguka, jamii tunayoiongoza na
watoto wetu, tuweze kuishi Maadili ya dini zetu.”
Nae Naibu Mkuu wa Hawza Imam Swadiq Sheikh Muhammad Abdu ambae
pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu ya T.I.C amewataka
Viongozi kuwatambua watu wanaowaongoza katika Dini zao na kuwasisitiza wasiwe
wabaguzi katika kutoa huduma kuangalia Imam ya watu wake.
“Sisi kama Viongozi jambo la kwanza tunatakiwa kuwa na Huruma
na Upendo kwa wale tunaowaongoza, kwani Kila kiongozi anaongoza watu wa aina
mbili ima atakuwa ni katika imani yake kama ni Mwislamu ana waislamu wenzie,
kama ni Mkristo ana wakristo wenzio, na akama sio katika dini atakuwa ndugu
yako katika Maumbile, yaani wewe ni binadamu nay eye ni binadamu inamaana
kwamba usije kuitumia nafasi yako katika kumbagua mtu yeyote katika wale
unaowaongoza” alisema Sheikh Abdu