Siku hii ya
leo ni siku inayokwenda sambamba na aya hii ya kufikisha ujumbe wa mungu siku
hii ya leo ni siku ambayo mtume wa Waislam sayyidina Muhammad (s.a.w.w)
alimtangaza Sayyidina Ali (a.s) kama Kiongozi baada ya yeye kiondoka duniani.
Siku hii ni
siku kubwa ambayo Waislam wote duniani na hususan Waislam Shia Ithnasheriya
siku hii wanaikumbuka kwa nguvu kubwa, lakini jambo la kujiuliza sisi leo
watanzania na wasiokuwa watanzania ni miaka zaidi ya 1400 sasa imepita
kunaumuhimu gani kwa kuikumbuka siku ambayo Sayyidina Ali (a.s) alitangazwa
rasmi kuwa Kiongozi wa Waislam baada ya Mtume kuondoka duniani?
Kuna vitu
muhimu au vigenzo vifuatvyo
Kitu cha
kwanza hiki nitakielekeza kwa waislam watanzania na wadunia ya kwamba umuhimu
wa Uongozi umuhimu wa usimamizi katika jamii yoyote ndio mafanikio yao katika mambo
, waislam duniani mara nyingi tumekuwa tunalingania sisi kuwa wamoja na kitu
kimoja, naamimi ya kwamba kuikumbuka siku hii ya kutangazwa Ali (a.s) kama
Kiongozi ni moja ya mafunzo muhimu kwa waislam ya kwamba.
Ndoto ya
sisi kuwa watu wamoja ni jambo linawezekana ndani ya jamii ya kiislam kwahivyo
siku ya Eid al Ghadir (Siku ya kutangazwa Sayyidina Ali (a.s) kuwa Kiongozi
baada ya Mtuem Muhammad (s.a.w.w) kuondoka duniani,ni darasa kubwa yakwamba
Waislam wakilienzi vizuri tukio hili
litawafanya wao wawe kitu kimoja na watakuwa na mzungumzaji mmoja na msemaji
wao.
Kwa lunga
nyingine waislam nao watakuwa na baba yao ambae anaweza kuwasemeaJambo la
pili ni kwanini sisi bado mpaka leo watanzania tunaikumbuka siku hii inaumuhimu
gani kwa watanzania, ukijaribu kulisoma tukio la kutawalishwa Ali (a.s) kama
kiongozi linabeba mapenzi aliyokuwa nayo mtume Muhammad (s.a.w.w).
ambayo mapezi
haya aliayaonesha katika ardhi ya makka kwa watu ambao hawakuwa waislam watu
ambao walikuwa wakiabudu masanam, mapenzi aliyaonesha mtume kwa watu wa makka ambao walikuwa ni mayahudi,
amapenzi aliyaonesha mtume kwa watu wa makka waliokuwa wakristo na akayaonesha
mapenzi haya kati yake yeye na dini zingine, mapenzi haya kwa siku ya leo anakabidhiwa Ali Ibn Abutalib (a.s) kama mrithi
wake.
Naamini ya
kwamba dunia na watanzania waslam na waisokuwa waislam mapenzi haya
wanayahitajia nadani ya nchi yao ya Tanzania na duniani kote.
Jambo
jingine muhimu kitendo cha kukabidhiwa Ali (a.s) kama msimamizi wa Uislam wa
Mtume baada ya yeye kuondoka duniani, Uislam wa Mtume ulikuwa uliogubikwa ni
amani, uliogubikwa nimaelewano, uliogubikwa ni kusikilizana na uliogubikwa ni
kuvumiliana kwa watu wenye fikra na mitazamo tofauti.
Siku hii ya
leo tunaposheherekea kutangazwa Ali (a.s) kama Kiongozi na mrithi wa mtume ni
siku ambayo Ali (a.s) anakabidhiwa rasmi Uislam huu wa Mtume, naamini ya kwamba
Watanzania waislam ,Wakristo na Mapagani naamini ya kwamba Uislam huu aliopewa
Ali (a.s) kutoka kwa mtume tunauhitajia.
Watanzania
leo hii na watu wote duniani wanayohaja ya mitazamo ya watu kukaa kwa amani,
kukaa na kuelewana, kukaa na watu na kuvumilaiana mitazamo hii inahitajika
kwenye siku hizi za sasa na kwenye muda huu.
Tanzania hii ambayo sote
tunakubaliana watu wake na maumbile yake na viongozi wetu waliopita
tunaovumiliana, hatujui mivutano ya kidini, ni watu hatujui mitizamo ya kifikra
ni watu kila mtu anamuheshimu mwenzake katika fikra na mitazamo yake.
Naamini ya
kwamba siku hii ya leo siku ya kutawalishwa Ali (a.s) ni siku ambayo tunausoma
Uislam huu wa kuienzi nchi yetu kubakia na amani na kuienzi nchi yetu kubakia
na maelewano..
Jambo la
mwisho niliseme ni muhimu katika Utawala na katika kukabidhiwa Ali (A.S) kama
Kiongozi dunia leo hii inakosa kitu kinachoitwa Uadilifu, Uadilifu ni jambo
lililopotea katika dunia hii tunaoishi leo, bali hata wale wanaodai ni
Waadilifu huenda kuna vigezo vingine uadilifu hakuna.
Naamini
yakuwa siku ya kutangazwa Ali (a.s) ni kukabidhiwa rasmi kitu kinachoitwa
uadilifu, na ninaamini Watanzania tunayohaja ya kuibakisha amani yetu na
utulivu wetu na uadilifu kufanyiwa kazi na kuwanacho katika jamii yetu.
Mtume
Muhammad (s.a.w.w) katika utawala wake na katika Uongozi wake jambo la usawa ni
jambo alilolitilia umuhimu mno, usawa huu aliokuwa nao mtume ndio aliokabidhiwa
Sayyidina Ali (a.s) siku ya leo, Ukimsoma Ali (a.s) katika maisha yake utampata
yakwamba katika utawala wake aliouchukua leo kwa mtume hakuwabagua watu pamoja
na tofauti za fikra na mitazamo yao.
alikuwa na watu wakimpinga alikuwa na watu
hawakubalianinae kifikra, walikuwepo watu hawamuamini kuwa yeye ni kiongozi,
lakini wote alikwenda nao sawa na kila mwenye haki yake alimpa watu wote aliona
ni sawa.
Siku hii ya
leo katika Uislam ni kuenzi maelewano kwa waislam na wasiokuwa waislam ni
kuenzi mapenzi yaliyokuwepo kati ya waislam na wasiokuwa waislam, ni kuenzi
usawa, ni kuenzi amani ni kuenzi utulivu.
Vile vile
tunatoa pole rasmi kwa ndugu zetu wale na tetemeko ya ardhi katika mikoa ya
kanda ya ziwa, ndugu zetu wote waliokubwa na balaa hili kwa kweli tunatoa pole
kubwa katika siku hii aliotawalishwa Ali (A.S) kama Kiongozi na tunawaomba
asasi za watu binafsi na watu wengine kuwaunga mkono kuwasaidia kwani nidio
jambo la ubinadamu na ambayo ndio jambo
ya dini zote linahimiza hivyo.
Na kama
vilevile hongera kwa mahujaji kwa kurudi salama na lakini tunatoa pole kwa
ndugu zetu ambao mwaka jana watu wengi walifariki katika ardhi ya minna, pia
tunatoa pole kwa ndugu zetu ambao walikosa ndugu zao katika tukio lile la mina
la kutisha na la ajabu.
Mwisho
Namuomba Allah / Mungu/ Mwenyezimungu (swt)
katika siku hii ya leo siku ya kutawalishwa Ali (A.S) kama Kiongozi
baada ya Mtume kuondoka duniani, iwe ni siku ya amani na iwe ni chachu ya
kuidumisha amani katika ardhi ya Tanzania, iwe ni sababu kubakia Tanzania kuwa
kisiwa cha amani.
iwe ni sababu kwa Viongozi wetu wa serikali wa awamu hii ya
tano kuwa na maelewano mazuri na wanaowaongoza na mungu aendelee kuwapa busara,
hekima na utulivu na swiha na afya waweze kuipeleka nchi mahala pazuri,
asanteni sana na hongereni kwa siku hii kubwa ya kutawalishwa Ali (a.s) kama
Kiongozi baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)
Na:Sheikh Hemed Jalala.
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia
Ithnasheriya Tanzania