Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema ni jambo la kawaida leo hii
ndani ya ardhi ya palestina kuvunjwa nyumba zao na haipiti siku mbili
inayokwenda kwa mungu nyumba za wapalestina zinavunjwa. Kwa hiyo wapalestina
wanamakubwa yanayowakabili, wanamengi mazito wanayowakumba.
Leo hii wapalestina wamekuwa wakizagaa duniani kwa kufukuzwa kutoka katika nchi zao na kwa bahati mbaya na ni jambo la kusikitisha wapalestina wanapofukuzwa katika nchi yao wanakuja kuchukuliwa watu kutoka mataifa tofauti wanapelekwa kuishi katika ardhi ya watu ambayo ni ardhi ya wapalestina.
“Huu ni uvamizi ambao haukubaliki,huu ni
ukandamizi ambao hatuwezi kuunyamanzia. Sisi kama waislam na kulingana na
itikadi ya kiislam kwamba, Uislam moja ya itikadi zake sio tu kujali mambo ya
waialsm tu bali ni kujali mambo ya wanaadam, na haya ndio mafunzo ya dini zote.
Sisi kama waislam na kama watanzania tunaomba palestina.
“Sauti yetu tunapoitoa bila shaka vyombo vya
umoja wa mataifa vinatuelewa, tunaomba vyombo vya umoja wa mataifa, tunawaomba
wanaadam, tunawaomba waislam,tunawaomba wasiokuwa waislam, wapalestina waishi
nawao kwa utulivu kamatunavyoishi sisi hapa Tanzania, wapalestina waishi kwa
amani kama tunavyoishi leo watanzania kwa amani” amesema Sheikh Jalala
“Wapalestina wakristo na waislam wakae vizuri na
dini zingine kama tunavyo kaa vizuri sisi watanzania. Tanzania inajulikana
kwamba ni kisiwa cha amani, ni mahala pa maelewano, katika historia yake ya
Tanzania haitambui ubaguzi na hivyohivyo palestina iwe ni mahala pa amani, iwe
ni mahala hapana ubaguzi, watu wote wakae pamoja, wakae kwa maelewano, dhulma
isambaratike, dhulma iondoke. Na hii ndio sababu kubwa ya sisi waislam wa
Tanzania kuikumbuka siku ya Palestina na pasikuwasahau hawa wapalestina ambao
ni Wakristo na Waislam” amesisitiza Sheikh Jalala