Sheikh Abdullatwif Issa Swalehe wa Bilal Muslimu Mission of Tanzania akielezea umuhimu wa maapizano kati ya mtume (s.a.w.w) na wakristo.
Habari Kamili
Waumini
wa dini ya Kiislam Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah leo wameungana na
Waislam wenzao ulimwenguni kote kusherehekea Ushindi wa tukio la
Mubahala, Sherehe hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Marehemu Sheikh
Dhikir Kihondo Temeke jijini Dar es Salaam.
Sheikh Hemed Jalala
amesema katika sherehe hiyo : kitendo cha Mtume (s.a.w.w) kutoka na
watu wanne na asiwachague watu wengine wakawaidia akakae meza moja na
Manaswara baada ya kushindwa Manaswara na Mtume (s.a.w.w) akaacha
kuwatoa manaswara katika ardhi ya Madina wakabakia kuishi katika mji wa
Najiran
Amesema Waislam watashinda Waislamu wataonekana
watendaji wazuri watakapokuwa wamekusanywa na mwamvuli wao mmoja Waislam
watakuwa tishio duniani na wataheshimiwa ndani ya nchi zao.
jalala amesema Watakapoitumia falsafa na hekima ya Mtume (s.a.w.w) ya kukaa na watu
ambao wanatofautiana nao kiitikadi wakakaa nao meza moja wakazungumza
nao Mtume (s.a.w.w) alikuwa na uwezo wa kuwafukuza Wakristo wa Najiran
.
Aidha amesema Mtume (s.a.w.w) alikaa nao meza moja akakaa nao Madina Mtume
(s.a.w.w.)hajawalazimisha Wakristo wa Najiran waingie katika Uislam
ambapo alikuwa na uwezo wa kunyanyua upanga na kuwaambia tamkeni shahada
mbili akuwalazimisha kwa sababu hakuna kulazimishana katika dini.
Amesema ni
makosa makubwa kuwepo fikra kwamba ni lazima kuwasilimisha watu kwa
nguvu wawe Waislam ni makosa makubwa hakuna katika Uislam, Uislam
hausemi ya kwamba twende tukawauwe watu hili wawe Waislam.
Ameongeza kuwa vita vyote
alivyopigana Mtume (s.a.w.w) vilikuwa ni vita vya kujilinda Warabu
walimkataza Mtume (s.a.w.w) asitangaze neno la Mungu kwa makatazo hayo
alipambana nao Mtume (s.a.w.w) hajatoka kuwapiga watu waingine.
"Wakristo wa Najiran waliposhindwa Mtume (s.a.w.w) hajawaambia kwamba
ingieni katika Uislam kwamba lazima muwe Waislam au nitawauwa bali Mtume
(s.a.w.w)" amesema Jalala.
Kasisitiza kuwa Mtume aliwaambia mkiingia katika Uislam mna haki zote kama Waislam
wengine wakawaida katika kumbukumbu ya kuukumbuka ushindi wa Mtume
(s.a.w.w) na Ahlul Bayt (a.s) kwa manaswara wa Najiran tujifunze hekima
hii kubwa ya kuvumilia kuweza kukaa pamoja na adui bali na mtu ambaye
unatofautiana naye kukaa katika meza moja
|