Friday, September 23, 2016

“Ukosefu wa Uongozi ni janga la Kila Jamii” Sheikh Swalehe


Sheikh Abdullatif Swaleh akizungumza jambo katika maadhimisho ya Eid al Ghadir, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
“Moja ya Majanga / Matatizo ambayo jamii  inayokabiliana nayo jamii ile iwe ni jamii ya Kidini, iwe ni jamii ya Kipagani, iwe ni jamii ya Kiislam, iwe ni jamii isiokuwa ya Kiislam, moja ya majanga makubwa ambayo inayokabiliana nayo ni swala zima la Uongozi.

Uongozi imekuwa ni janga la kimataifa, limekuwa ni janga la Kidunia, hakuna jamii isipokuwa inahitajia  Uongozi, hakuna jamii isipokuwa inahitajia Uongozi tena Uongozi ambao wenye hekima,uongozi wenye busara, uongozi wenye utambuzi yakinifu kwa kila linaloendelea katika jamii husika”

Na. Sheikh Abdullatwif Swalehe
#Eid al #Ghadir2016

“Malengo ya Nabii Issa / Yesu (a.s) na Imam Mahdi (a.s) ni kujaza Amani Dunia” Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akihutubia Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
Na ndio maana tunapong’ang’ania kwamba sisi Watanzania jambo la Uongozi linatukusanya sisi sote kama Watanzania pasina tofauti za dini zetu, na wala waislam wasije wakaja wakadhania kuna siku watakuja kuwabadilisha watanzania wote wawe waislam hiyo haitotokea hata siku moja na wala ndugu zetu Wakristo wasije wakaja wakadhania kuna
siku watatuhubiria sote tukamuacha Muhammad Ibn Abdillah (s.a.w.w) na tukamfuata Yesu (a.s) haitotokea,kwahiyo kilichobakia ni sisi kuvumiliana ndani ya nchi moja na kama dungu wamoja. 

Kumbe mwisho wetu Nabii Issa / Yesu (a.s) ataswali nyuma ya Imam Mahdi (a.s).Malengo ya Nabii Issa / Yesu (a.s) na malengo ya Imam Mahdi (a.s) ni mamoja ni kuijaza dunia amani, maelewano, masikilizano na mshikamano.

Na.Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania
#KhutbayaIjumaa2016

“Inashangaza jamii ya Kiislam hakuna Hospitali na Shule zinazotoa huduma Bure” Sheikh Swalehe

Sheikh Abdullatif Swaleh akizungumza jambo katika maadhimisho ya Eid al Ghadir, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
“Ni jambo la Kushangaza katika jamii yaWaislam kuna Hospitali nyingi yako chini ya Waislam lakini ni Binafsi, lakini sijawahi kuona kuna Hospitali kwamba hii Hospitali ni ya Waislam wote katika hii Tanzania yetu, Sijui kuna Hospitali ambayo ni maalumu Kuwa Hospitali hii ni ya Waislam,

Mwislam anaenda kutibiwa bure,mwislam anatatizo lake,vipimo anaenda kupimwa bure, ikiwa inahitajika tiba anatibiwa bure, Waislam wote tukitaka tujue ni majanga ya namna gani tunayokabiliana nayo kutokana na ukosefu wa kuwa na Uongozi, tena Uongozi imara,uongozi madhubuti, 

uongozi wenye hekima  busara na utambuzi ya kinifu unaojua kwamba ni jambo gani linaloendelea katika ulimwengu,na sisi kama wa wanajamii ya jamii Fulani kama Waislam tunahitajika tufanye nini?

Waislam hatuna Hospitali, Waislam hatuna Shule ni Waqf kwa Waislam kiasi kwamba Mwislam yeyote angienda kusoma bure hatuna, lakini tuna Shule za watu binafsi, hivi tujiulize wale watu binafsi wanapesa nyingi kuliko sisi Waislam wote pindi tukiunga na jibu ni hapana, lakini kukosekana Uongozi katika jamii ndio sababu inayopelekea kukosekana huduma hizo katika jamii.ndio sababu iliyopelekea kukosekana huduma hizo katika Jamii”Sheikh Swalehe.

Sheikh Abdullatwif Swalehe
#Eid al #Ghadir2016

“Nabii Issa / Yesu (a.s) atashirikiana na Imam wa Waislam Imam Mahdi (a.s)” Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akihutubia Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
“Imam Muhammad Ibn Hassan Al-#Mahdi (a.s) atakapodhihiri kwa itikadi ya Waislam wote, Nabii Issa Ibn Mariyam / Yesu (a.s) nay eye atashuka, katika Kitatu cha Swahihi Muslim tunasoma hadith inayosema Waislam mtakuwa na hali gani? Wakati Nabii Issa Ibn Mariyam / Yesu (a.s) na Imam wenu yupo ndani yenu, Nabii Issa Ibn Mariyam / Yesu (a.s) atashuka,Nabii Issa / Yesu (a.s) atashirikiana 

na Imam wa Waislam Imam #Mahdi (a.s)  swala itakimiwa, Imam Mahd (a.s) atamwambia Nabii Issa / Yesu (a.s) atangulie aswalishe, Nabii Issa / Yesu (a.s) atasema Laa/ Hapana / atakataa na atasema zama hizi sio zama zangu, Hapo Imam wa Waislam Imam Mahdi (a.s) atatangulia mbele na Nabii Issa / Yesu (a.s) ataswali nyuma ya Imam Mahdi (a.s) Huu ndio mwisho wa Waislam na Wakristo,”.

Na.Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania
#KhutbayaIjumaa2016