Friday, June 26, 2015

Polisi auwa Mama mzazi Pemba

Askari wa Jeshi la Polisi Said Kombo anayefanyia kazi katika kituo cha Polisi Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba anashikiliwa na jeshi la Polisi  kwa tuhuma za kumuuwa mama mzazi kwa kumchoma kitu chenye ncha kali .

Askari huyo   ambaye anadaiwa kuwa ni mgonjwa wa akili ametekeleza kitendo hicho jana majira ya saa tano za asubuhi ambapo inadaiwa kuwa alimchoma mama mzazi Mwanaisha Haroun Hamad .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi daktari wa  zamu katika Hospitali ya Micheweni Mkubwa Habib amekiri kupokea mwili wa marehemu huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake .

 Amefahamisha kwamba marehemu huyo alikuwa amepata majeraha sehemu za mgongoni , mikononi na kifuani na kuongeza kifo chake kimetokana na kutokwa damu nyingi .

“Ni kweli nimepokea majeruhi ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali , na alipofikishwa hapa alikuwa hana tana fahamu ”alifahamisha .

 “Baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wake nilibaini kuwepo na majeraha sehemu za mgongoni , mikononi pamoja na kifuani ambapo alikuwa anatoka damu katika mwili wake ”aliongeza

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walisikia kelele na walipofika wakimkuta marehemu akiwa anatoka damu sehemu za mwili na walichukua hauta za kumpeleka hospitali kabla ya kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi .

“Mimi niliskia kelele na nilipofika nilimkuta anatoka damu nyingi na tuliamua kumpeleka hospitali kwanza kupata matibabu na baadaye tulipeleka taarifa kwa jeshsi la Polisi ”alieleza mmoja wa wananchi akiwa hospitalini hapo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishina Msaidizi Shekhan Mohammed Shekhan amesema kuwa mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua za upelelezi.

Alieleza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linendelea  kumuhojiwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya kukamilisha taratibu na badae kumfikisha mahakamani kwa taratibu za kisheria zaidi dhidi yake.


“Baada ya tukio kutokea Askari wa Jeshi la Polisi walimkamata mtuhumiwa na kwa sasa tunaendelea kumhoji na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinamkabili upelelezi utakapo kamilika ”alieleza Kamanda Shekhan .

Hata hivyo kamanda Shekhan amewataka wananchi wanaosihi na wagonjwa wa akili kuwapeleka Hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na kuacha kuwafungia ndani ili kuwalinda na madhara yanayoweza kuwapata 
Chanzo Habari24.net

Mawlana Sheikh Hemed Jalala amenya Viazi Mbatata

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalalala akiwa anawasaidia wanaharakati na Wanafunzi wa Hawzat Al- Imam Swadiq (a.s) kumenya Viazi Mbatata, Kigogo-Post Dar es salaam. katika maandlizi ya chakula cha Futari.








Sheikh Jalala "Falsafa ya Ramadhani ni Waislam kuwa na Umoja"


Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikha Hemed Jalala akitoa khotuba ya Ijumaa ya 9Ramadhani, Msikitini Ghadir Kigogo-Post Dar es salaam.



Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa wanaomba dua ya Umoja baada ya Swala ya Ijumaa.
 Habari Kamili
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala amesema Kama Mashia na Masuni wakikaa pamoja katika kujadili maendeleo ya Uislam, mafanikio makubwa yatatokea.
 Hayo ameyasema leo katika Khutba ya Swala ya Ijumaa ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1436, sawa na 26/06/2015, ikiwa ni ramadhani ya 9.Ila kasisitiza kwa kuacha tofauti tulizokuwa nazo.
Mawlana Sheikh Jalala amesema Ramadhani ni Madrasa kubwa sana inayotufundisha Umoja, Ummoja wa watu na Waislamu kwani Moja ya jambo linalofurahisha ni kufaradharishiwa watu wote kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Moja ya falsafa ya kufaradhirishiwa watu waliopita na walioopo kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani ni swala la umoja.Ibada ya mwezi wa ramadhani unatufundisha kusahau tofauti zetu na kuwa na jambo moja katika jamii yetu”amesma Sheikh Jalala.
Amesema Mtume alipoingia madina kitu cha kwanza alichokifanya ni kutengeneza umoja,Umoja uliokuja kutengenezwa na Mtume kati ya Muhajirina na Aswar ndio iliyotengeneza Serikali ya Kiislam Darasa la ramadhani inatufundisha kuacha tofauti zetu na kuwa kitu kimoja.
Hatahivyo amesema Waislam ndio waathirika wakubwa katika umasikini uliokithiriMadrasa ya ramadhani ni kuondoa matatizo katika jamii, bila ya kuacha tofauti zetu hatutofikia malengo ya Ramadhani.




Madhara 10 ya vidonge vya kupanga uzazi kuzuia mimba.

Vidonge vya Uzazi wa Mpango, ni moja ya njia inayopendekezwa na Wataalamu wa Mpango wa Uzazi katika kuzuia mimba. Hata hivyo, vidonge hivyo vinaweza kutimiza malengo hayo ya mpango huo ikiwa tu vitatumiwa vizuri na kwa usahihi, kwa sababu tafiti zilizopo, zinaonyesha kwamba asilimia nane (8%) ya wanawake hupata mimba zisitarajiwa kila mwaka, huku wakiwa katika mpango huo kutokana na baadhi yao kujisahau kumeza vidonge hivyo.
Kwa mujibu wa tafiti hizo ambazo FikraPevu inazo, vidonge hivyo vya mpango wa uzazi vikitumiwa vizuri, kwa kuhakikisha muda wa matumizi yake unakuwa ule ule, ni mwanamke mmoja pekee kati ya 100 anayeweza kupata mimba isiyotarajiwa ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi ya dawa hizo.

Hadi sasa kuna aina kuu mbili tu za vidonge vya uzazi vinavyotumiwa na wanawake katika wa mpango huo, ingawa aina zote hizo zina vichocheo (hormons). Aina hizo kitaalamu zinaitwa Estrogen na Progesteron. Estrogen ni aina ya kichocheo kinachotengenezwa na uterasi/kizazi, kinachosaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi, kwa kuongoza ukuaji wa kuta za uterasi kwenye sehemu ya kwanza ya mzunguko wa hedhi.

Kwa upande wake, Progesterone, hiki ni kichocheo cha kopasi luteamu ya ovari, kinachosaidia kuanzisha mabadiliko katika endometriumu baada ya ovulesheni.

Ingawa katika aina hiyo mbili ya vidonge, kuna vingine vina kichocheo cha aina moja tu, kwa maana ya ama Estrogen au Progesterone, huku vingine vikiwa na vichocheo vyote viwili hivyo, lakini vidonge vyote hivyo ni salama, na vinafanya kazi kwa kufanya ute mzito kwenye shingo ya mji wa mimba na kuzuia kupevuka kwa yai, hivyo kuzuia mimba kwa kiwango cha asilimia 99.

Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza pia kutumika kama tiba ya kuweka sawa mzunguko wa hedhi, kuzuia maumivu makali wakati wa hedhi, kutibu chunusi pamoja na kupunguza hatari ya magonjwa katika via vya uzazi, ambayo hayatokani au kusababishwa na magonjwa ya ngono.

Hata hivyo, pamoja na usalama wa vidonge hivyo katika kufanya kazi yake hiyo ya kuzuia mimba na tiba kwa magonjwa hayo, vidogo hivyo vinaweza kumsababishia athari za kiafya mwanamke kama havitumiki katika mpangilio sahihi.

  1. Athari kuu 10 zinazoweza kusababishwa na vidonge hivyo ni pamoja na kutokwa na damu ukeni baada ya hedhi ya kawaida. Kwa mujibu wa wataalam wa mpango huo, athari hiyo huweza kuwapata asilimia 50 ya wanawake wote wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango. Hali hii huweza kuwatokea ndani ya miezi mitatu baada ya kuanza matumizi ya dawa hizi. Kwa ujumla, hali hiyo huweza kukoma kwa zaidi ya asilimia 90, pindi mwanamke anapoanza kutumia pakti ya tatu ya dawa hizo katika kipindi hicho cha kutokwa damu ukeni. Mwanamke anapotokewa na hali hiyo kwa mfululizo wa siku tano au zaidi baada ya kumaliza siku zake za kawaida za hedhi, anashauriwa kuwasiliana na mhudumu wa afya wakati akiendelea kutumia dawa hizo.

  2. Athari ya pili, ni kujisikia kichefuchefu. Mara nyingi hali hiihumtokea mwanamke mwanzoni tu baada ya kuanza kumeza vidonge vya uzazi wa mpango, ingawa hali hii inaweza kukoma baada ya siku chache. Inashauriwa pia kwa mwanamke anayepatwa na hali hii ya kichefuchefu kuwasiliana na mhudumu wa afya kama ataona hali hiyo inazidi. 

  3. Matiti kujaa au kuwa na maumivu, ni athari nyingine inayoweza kusababisha na matumizi ya vidonge hivyo. Hali hii huweza kumpata baada ya kuanza kutumia vidonge hivyo, na huweza kukoma ndani ya wiki moja tu. Hata hivyo, inashauriwa kwamba ikiwa matiti hayo yatatokwa na uvimbe au maumivu yasiyoisha, ni muhimu kutafuta tiba kwa wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya kinywaji chenye kafeini (caffeine) na chumvi na kuvaa brauzi isiyobana matiti.

  4. Maumivu ya kichwa ni athari nyingine inayoweza kumtokea mwanamke, ingawa pia kuumwa kichwa kunaweza kuwa na dalili za magonjwa mengine. Hata hivyo, kama itatokea maumivu hayo ya kichwa yakaanza tu mara baada ya kumeza vidonge hivyo, hiyo itakuwa ni dalili ya athari mojawapo na ni vyema kutoa taarifa kwa mhudumu wa afya.

  5. Vidonge vya uzazi wa mpango huweza pia kuongezeka uzito wa mtumiaji, ingawa tafiti nyingine zimeshindwa kuthibitisha uhusiano kati ya vidonge hivyo na mabadiliko ya uzito wa mtumiaji. Aidha, baadhi ya wanawake hupatwa na tatizo la maji kuganda kwenye matiti na maeneo ya nyonga baada ya kutumia vidonge hivyo. 

  6. Mabadiliko ya hisia huweza pia kumtokea mwanamke anayeanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Inashauri kwamba pindi mwanamke anapoona dalili hii, ni muhimu kumjulisha mhudumu wa afya ili kuweza kujadili ni jinsi gani ataweza kutumia dawa hizo, kwa sababu dalili hii ni mbaya kiafya kwa mtu mwenye historia ya ugonjwa wa Kushuka Moyo (Depression).

  7. Athari nyingine ya dawa hizi ni kutokwa na uchafu ukeni. Baadhi ya wanawake, mara tu baada ya kutumia vidonge hivi hutokwa na uchafu ukeni, ikiwa ni pamoja na kupatwa na uwezekano wa kupungua au kuzidi kwa ute wakati wa tendo la ndoa. Ni muhimu sana mwanamke anapobaini dalili hizi, kuonana na mhudumu wa afya ili kubaini kama hali hiyo imesababishwa na athari ya vidonge au kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

  8. Wanawake wengine huweza kujikuta wakikosa siku zao za hedhi baada ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Ingawa ugonjwa wa msongo wa mawazo (stress), magonjwa, mchoko wa safari unaweza kusababisha hali hii, lakini inashauriwa kupima kama mtu amaepatwa na ujauzito hata kama anatumia vidonge hivi kama itatokea kukosa hedha katika mazingira tata.

  9. Kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni athari nyingine inayoweza kumkuta mwanamke anayetumia vidonge vya uzazi wa mpango kutokana na vichocheo vilivyomo ndani ya dawa hizo, ingawa pia magonjwa kama ya kisukari, shinikizo kubwa la damu na kadhalika yanaweza pia kuchangia tatizo hilo.

  10. Athari ya 10 na ya mwisho kwa wanawake wanaotumia vidonge hivyo, ni mabadiliko ya taswira ya kitu anachokiona mbele yake, hasa kwa wanawake wanaovaa miwani ya macho. Kwa kuwa macho ni moja ya eneo muhimu la ufahamu kwa mwanadamu, hali hii inapowapata wanawake, inashauri kuonana mara moja na daktari wa macho pindi tu dalili hizi zinapoanza kujitokeza. 

Ni tahadhari gani mwanamke anatakiwa kuchukua kabla na baada ya kuanza matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango?

Kwa mwanamke mzazi, hairuhusiwi hata kidogo kuanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ndani ya wiki tatu tu baada ya kujifungua mtoto au ikiwa atakuwa ananyonyesha mtoto mwenye umri wa chini ya miezi sita.

Aidha, ikiwa mwanamke amefanyiwa upasuaji mkubwa wa aina yoyote katika siku za karibuni, au kama mwanamke husika ni mvutaji wa sigara na ana umri wa zaidi ya miaka 35, haruhusiwi kutumia vidonge hivyo, kama ambavyo pia haruhusiwi kufanya hivyo mwanamke mwenye historia ya ugonjwa wa ini, manjano, moyo, saratani ya matiti, tumbo la uzazi pamoja na shinikizo la damu linalobadilikabadilika kila wakati kwa viwango vya 140/90 mmHg au zaidi, na au kama ana historia ya maumivu makali ya kichwa.

Fatuma Mwiru amepata Baraka Kubwa.

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala katikati, kulia kwake ni baba mzazi wa Fatuma Mwiru na kushoto kwake ni Sheikh Muhammad Abdi wakikaribia nyumbani kwao Fatuma Mwiru.
Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongozana na Sheikh Muhammed Abdi,Muhammed Juma, Mwenyekiti Ammar na Alhaj Mputa, waliweza kufanya Ibada ya Swala, Futari na kumaliza kwa Dua nyumbani kwa mzee Mwiru
  
Fatuma Mwiru ni mmoja wa Wanaharakati wakubwa na sasa ameshachukuwa Fomu ya Kugombea Udiwani katika Kata ya Kisarawe, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Sheikh Muhammad Abdi akiongoza swala ya Jamaa Nyumbani kwa Mwanaharakati Fatuma Mwiru.


Mawlana Sheikh Hemed Jalala katikati, kushoto ni Ammar na Kulia ni Salum wakiwa pamoja wakiomba Dua katika swala ya Magharibi iliyoswaliwa kwa mzee Mwiru nyumbani kwao kwa Fatuma Mwiru

Sheikh Muhammad Abdi akipakua chakula cha Futari katika sahani lake, katikati ni Sheikh Saidi na Kulia kwake ni Ammar

Sheikh Muhammed Juma katibu, akijisevia chakula katika muda wa futari

Mawlana Sheikh Hemed Jalala akichukua chakula cha futari.

Katikakati ni Alhaji Mputa,kulia kwake ni Mzee Mwiru baba yake na Fatuma Mwiru.

Sheikh Saidi akimpokea Mawlana Sheikh Hemed Jalala huko kisarawe Jana majira ya Jioni.

Sheikh Jalala "Jamii ipambike na Ukweli na Uadilifu"






Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala amesema lengo kuu la Mwenyezimungu kuuleta mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kuleta mabadiliko katika jamii.
Alisma Moja ya kuleta mabadiliko katika jamii ni kuondoa unyonyaji, umasikini, ufisadi,uongo na hali mbaya ya masha ya mwanaadamu.
“Jamii yetu ikitaka kubadilika ni lazima ipambike katika sifa kuu mbili yaani Ukweli na Uadilifu” alisema Sheikh Jalala
Hayo aliyasema jana katika kipindi cha live katika television ya chanel ten, iliyo Dar es salaam, katika kipindi kilichoongozwa na Muhammed Iddi cha Ramadhani Karim.
“Na hakuna jambo mbaya zaidi mbele ya Mwenyezimungu kama kuifanyia Jamii hiyana” alisema Sheikh Jalala.
Aidha alisema mabadiliko ya mja ni lazima awe na huruma kwa mayatima na  wanyonge, kwani daima wema huo haupotei mbele ya mwenyezimungu ( swt) na nilazima kumtegemea muumba wa mbingu na ardhi.