Wednesday, November 2, 2016

Miezi 12 ya kujifunga mkanda yaja



Rais John MagufuliDodoma. Wakati Serikali imewasilisha bungeni sura ya bajeti ya 2017/18 inayoonyesha matumizi ya Sh32.9 trilioni, wananchi watatakiwa kufunga mkanda zaidi baada ya kutajwa mambo 14 yatakayowekewa nguvu kubana matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.

Sura hiyo ya bajeti ijayo inaonyesha ongezeko la Sh3.4 trilioni ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 ya Sh29.5 trilioni iliyosomwa bungeni Juni ambapo asilimia 40 ya bajeti hiyo, ilielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Bajeti inayotekelezwa sasa ilipunguza mambo mengi yasiyo ya lazima ikiwamo safari za viongozi za nje ya nchi, semina na kuna wakati Rais John Magufuli alifuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo la kuokoa fedha kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.

Jana, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha mpango huo aliongeza maumivu 14 kutokana na uamuzi wa Serikali kuendelea kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa mwaka ujao.

Haki za Binadamu yawakingia kifua waandishi

Mratibu wa Muungano wa Watetezi wa Haki zaDar es Salaam. Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umelitaka Jeshi la Polisi nchini kubadilisha mtazamo na kuwaona waandishi wa habari kama wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza leo (Jumatano), wakati wa warsha maalumu ya kujadili usalama wa waandishi wa habari, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengulumwa amesema polisi hawana mwamko katika kuwalinda waandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao bali wao ndiyo wanaohatarisha usalama wao.

Amesema jeshi la polisi lina uwezo wa kulinda usalama wa waandishi wa habari lakini mwamko wao ni mdogo, hivyo wanahitaji kupata mafunzo maalumu ya kuwawezesha kubadili mtazamo wao juu ya tasnia ya habari.

"Tumeona katika nchi mbalimbali kwamba polisi hawawapendi waandishi wa habari. Hilo linatokana na mawazo hasi waliuonayo juu yao, tunahitaji kutoa elimu kwao ili watusaidie kuwalinda waandishi wanapotekeleza wajibu wao," amesema Olengulumwa.

Tanzania yashika nafasi ya pili utoaji huduma za kifedha

Dar es Salaam. Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa  kutoa huduma za kifedha kwa wateja wenye kipato cha kati na  cha chini.

Taarifa zilizotolewa na Shirikisho la Asasi za Huduma za kifedha Tanzania (Tamfi) zinaeleza kuwa kwa Tanzania huduma za kifedha zinawafikia wananchi 3,800,000.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari leo, Mwenyekiti wa Tamfi, Joel Mwakitalu alisema Tanzania imeshika nafasi ya pili kati ya nchi tano za Umoja wa Afrika Mashariki.
Nchi ambazo zilikusanywa taarifa ni kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.

Nchi ya kwanza imetajwa kuwa ni Kenya ambayo inawafikia watu milioni nne kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa mwaka 2014 katika nchi zote za EAC huku Tanzania zikisimamiwa na Shirikisho la Asasi za Huduma za kifedha Tanzania (Tamfi).


Mwakitalu alisema kinachosababisha huduma za kifedha  kutowafikia wateja wengi ni miundombinu kushindwa kuwafikia walio vijijini.

"Tumekutana na wenzetu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India kujadili ni namna gani huduma za kifedha zitawafikia wananchi wengi kupitia vikundi vidogovidogo kama Vicoba na vinginevyo kwakuwa vinawagusa sana wananchi wenye kipato kidogo," amesema Mwakitalu.

Dehqani: Uvamizi wa Wazayuni ndio tishio kubwa la usalama wa dunia

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, uvamizi na ukaliaji mabavu wa Wazayuni ndio tishio kubwa zaidi la usalama na amani ya dunia.

Ghulam Hussein Dehqani, amesema hayo katika kikao cha kila mwaka cha kamati ya nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo sambamba na kuashiria kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu  vya utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina amesema kuwa, uvamizi na ukaliaji mabavu wa Wazayuni dhidi ya ardhi za Palestina ndio tishio kubwa zaidi la amani na usalama wa dunia.

Amesema kuwa, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za kilimwengu kwa ajili ya kukabiliana na hatua hizo za utawala dhalumu wa Israel.
Athari za hujuma za kijeshi za Israel huko Gaza
Balozi na Naibu Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa sambamba na kukumbusha kushadidi vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji ya Israel dhidi ya wananchi madhulumi wa Palestina pamoja na hali yao mbaya amebainisha kwamba, kuna haja ya kuongezwa mashinikizo ya jamii ya kimataifa dhidi ya utawala huo ghasibu ili uhitimishe vitendo na hatua zake zisizo za kisheria dhidi ya wananchi wa Palestina.

Ghulam Hussein Dehqani amesema kuwa, mazingira mabaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ambayo yametokana na kuendelea mzingiro dhidi yao na vikwazo vya kiuchumi yamepelekea hali ya eneo hilo kuchukua mkondo mpana zaidi.