Dodoma. Wakati Serikali imewasilisha bungeni sura ya bajeti ya 2017/18 inayoonyesha matumizi ya Sh32.9 trilioni, wananchi watatakiwa kufunga mkanda zaidi baada ya kutajwa mambo 14 yatakayowekewa nguvu kubana matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Sura hiyo ya bajeti ijayo inaonyesha ongezeko la
Sh3.4 trilioni ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 ya
Sh29.5 trilioni iliyosomwa bungeni Juni ambapo asilimia 40 ya bajeti
hiyo, ilielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Bajeti inayotekelezwa sasa ilipunguza mambo mengi yasiyo ya lazima ikiwamo safari za viongozi za nje ya nchi, semina na kuna wakati Rais John Magufuli alifuta baadhi ya sherehe za kitaifa kwa lengo la kuokoa fedha kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.
Jana, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha mpango huo aliongeza maumivu 14 kutokana na uamuzi wa Serikali kuendelea kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa mwaka ujao.

No comments:
Post a Comment