Kinara wa Standard Chartered Mumbai Marathon ambaye pia ni Balozi wa Kampuni ya Multicjoice Tanzania wakwanza kulia Mr. Alphonce Simbu |
Na: Amina Kibwana
Kinara
wa Standard Chartered Mumbai Marathon ambaye pia ni Balozi wa Kampuni
ya Multicjoice Tanzania Alphonce Simbu amewasili jijini dar es salaam na
kueleza yaliyojiri katika mbio hizo.
Akizungumza na
waandishi wa habari, Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mh
Nape Nnauye ametoa shukurani zake kwa Multichoice Tanzania ambao ni
wafadhili wa mwanaridha huyo kwa msaada waliompatia pamoja na pongezi
za dhati kwa mwanaridha huyo kuchukua ushindi katika mashindano hayo
ambayo yalikuwa na washindani kutoka nchi tofautitofauti,
"Ninawashukuru
sana dstv kwa kujitolea kwao pale wanapoona kunafaa kwani mafanikio ya
Simbu yamepatikana kwa kupitia msaada huo na kuufanya mchezo huu kurudi
tena kwa kasi nchini kulinganisha na awali."
Naye
Katibu Mkuu wa chama cha riadha Nchini Willelm Gidabuday amesema kuwa
waliamchagua Alphonce kwa kuamini kuwa nanweza na atafanya vizuri katika
mchezo huo na kuweza kuiwakilisha vizuri Nchi yetu kutokana na kuweza
kufanya vizuri katika mashindano yaliopita.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema
kuwa wanaendelea kumdhamini Simbu na kwamba wanatarajia kuwa atafanya
vema katika michuano ijayo ya London Marathon ya mwezi April na yale ya
Dunia ya mwezi Agosti na kutuwakilisha tena kama alivyofanya huko mumbai
nchini India.
"Tunaendela kumdhamini Simbu na
tunashirikiana kwa karibu na meneja wake na kocha ili kuhakikisha kijana
anajinoa vizuri kwa ajili ya mashindabo yanayomkabili." amesema Ronald.
Kwa upande wake Mwanaridha huyo amewasifu waandishi wa habari kwa kazi walioifanya ya kutoa taarifa
kwa umma kuhusu yaliyojiri huko Mumbai wakati wa mashindano hayo pamoja
na Ufadhili alioupata kutoka Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kwa
kumuwezesha kufanya maandalizi mazuri yenye kiwango kinachohitajika.
Simbu
amesema kuwa katika mashindano hayo ushindani ulikuwa mkubwa sana kwani
wengi wa wanariadha walioshiriki walikuwa ni wazoefu na wenye sifa za
kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa.
Hata hivyo ameimba serikali
kukusanya wachezaji wengi katika mchezo huo kama wanavyofanya nchi
nyingine kwani kwenye 10 bora kulikiwa na wakenya 7 ,waethiopia 2 na
Mtanzania alikuwa
peke yake, hii inaleta ugumu sana kwenye mashindano kwani kwa kawaida
mkiwa wengi kuna mbinu za kusaidiana ilimradi kuhakikisha anashinda mtu
aliyekuwa katika tumi yenu". amesema Simbu.