Monday, July 20, 2015

RASMI--MOSES MACHALI WA NCCR KUPOKELEWA ACT KESHO

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ,kesho julai 21 atampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses  Machali(NCCR-Mageuzi), ambaye atajiunga atatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.


Machali ataambatana na Madiwani wawili,Kamishna  wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini.,
Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea na makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini  yenye jumla ya kata 15 za uchaguzi
Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni pamoja na wenyeviti wa matawi  101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali 648.wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini
Baada ya Mapokezi hayo ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo, Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ataelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi na madiwani kutoka vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya jumamosi julai 25.
Julai 26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi
Wakati kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya, jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vvama tofauti.

Abdallah Khamis
Afisa Habari -ACT-Wazalendo.
 Imetolewa leo julai 20/2015

Darsa la kwanza la Ujue Ushia-Tanga, Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akisalimiana na Waumini katika Mkoa wa Tanga ya Lushoto.
Muhadhara wa UJUE USHIA kwa mara ya kwanza ulianzia
 Mkoani Tanga wiliya ya Lushoto huko Mlalo mwaka 2012 
chini ya Uongozi wa Sheikh Hemed Jalala, kazi hiyo ilileta
 muamko mkubwa mno kwa wafuasi wa dini ya Kiislam 
Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah pamoja na 
Madhehebu ya Sunni, ilipofika tarehe 17/06/2012 Uongozi 
wa harakati za UJUE USHIA chini ya Sheikh Hemed Jalala 
 ulifanikiwa kuitisha mkutano mkubwa wa Mashia 
wanaoishi 
Dar es Salaam kwa ajili ya kutambuana na kujadili 
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Kishia Tanzania.
Tunaweza kuona ni kwa mda mchache sana jamii ya Kishia iliweza kutembea katika sehemu mbalimbali na kufikisha ujumbe halisi wa dini ya Kiislam aliyouacha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), tunajukumu kubwa la kuitunza kazi hii iliyoanzishwa na waasisi hawa. Tusikubali hata siku moja mtu atushawishi kuivunja kazi hii ambayo imetuletea heshima katika jamii yetu
Kiongozi huyo akiwa katika Darsa la Ujue Ushia na waumini wa Mkoa wa Tanga

Wakwanza kulia ni Alhaji Sheikh Mputa akiwa makini kusikiliza Darsa la Ujue Ushia

Wapili kushoto ni Mwanaharakati wa Afroshia Mr. Ibrahim Mpiripiri akijumuika na wenzake katika kusikiliza darsa hilo

Sheikh Salim Mwamba akiwa msitari wa mbele katika kuwaelewesha waumini wa Dini ya Kiislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya

Sheikh Hoza akiteta jambo na wazee wa Mji huo huko Tanga ya Lushoto