KIONGOZI
wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ,kesho julai 21 atampokea Mbunge
wa Kasulu, mjini Moses Machali(NCCR-Mageuzi), ambaye atajiunga
atatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.
Machali
ataambatana na Madiwani wawili,Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake
pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu
mjini.,
Pia
katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea
na makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini yenye jumla ya kata 15 za
uchaguzi
Mbali
na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama
cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni pamoja na wenyeviti
wa matawi 101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali
648.wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika Chama cha
NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini
Baada
ya Mapokezi hayo ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo, Kiongozi wa Chama
Zitto Kabwe ataelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi
na madiwani kutoka vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya
jumamosi julai 25.
Julai
26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika
majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi
Wakati
kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya,
jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa
na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vvama
tofauti.
Abdallah Khamis
Afisa Habari -ACT-Wazalendo.
Imetolewa leo julai 20/2015
No comments:
Post a Comment