Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akisalimiana na Waumini katika Mkoa wa Tanga ya Lushoto.
Muhadhara wa
UJUE USHIA kwa mara ya kwanza ulianzia
Mkoani Tanga wiliya ya Lushoto
huko Mlalo mwaka 2012
chini ya Uongozi wa Sheikh Hemed Jalala, kazi hiyo
ilileta
muamko
mkubwa mno kwa wafuasi wa dini ya Kiislam
Madhehebu ya Shia Ithna
Ashariyyah pamoja na
Madhehebu ya Sunni, ilipofika tarehe 17/06/2012
Uongozi
wa harakati za UJUE USHIA chini ya Sheikh Hemed Jalala
ulifanikiwa kuitisha mkutano mkubwa wa Mashia
wanaoishi
Dar es Salaam
kwa ajili ya kutambuana na kujadili
changamoto mbalimbali zinazoikabili
jamii ya Kishia Tanzania.
Tunaweza kuona
ni kwa mda mchache sana jamii ya Kishia iliweza kutembea katika sehemu
mbalimbali na kufikisha ujumbe halisi wa dini ya Kiislam aliyouacha
Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), tunajukumu kubwa la kuitunza kazi hii
iliyoanzishwa na waasisi hawa. Tusikubali hata siku moja mtu atushawishi
kuivunja kazi hii ambayo imetuletea heshima katika jamii yetu |
No comments:
Post a Comment