Friday, May 8, 2015

Tuwasaidie Wahanga wa Mafuriko

Hali ya Mvua katika jiji la Dar es salaam.athari ya mafuriko:baadhi ya nyumba za watu zikiwa zimezingirwa na maji

Maulana Sheikh Hemedi Jalala: Imam wa Masjid Ghadiir Kigogo Post-Dar es salaam
 Katika khutba ya leo ijumaa tarehe 8/5/2015, katika masjid Ghadiir –kigogo Dar es salaam, Maulana sheikh Hemedi Jalala amewataka waislaam, waumini na jamii  kwa ujumla, kuwasaidia na kuwaenzi  watu waliokumbwa na mafuriko, 

alisema:          ” sehemu kubwa ya Jiji la Dar es salaam limekumbwa na mafuriko na mvua kubwa, zilizosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha na wengine kukosa makazi na malazi, ni wajibu wetu kuwasaidia , kwa sababu ni ndugu zetu,na jamaaa zetu,  tufahamu yakua tukio lolote linalotokea duniani  lina maagizo ya  mwenyezi mungu”. 

Maulana aliendelea kusema, “kuwasaidia waliopatwa na matatizo ni katika ibada, ibada ni tukio lolote linalomkurubisha mtu na mungu, kuondoa adha, miba, chupa, misumari njiani, ni ibada , navilevile kuwasaidia, kuwapa pole, 

kuwatembelea na kutoa misaada ya kihali na mali na kuwafariji ni ibada kubwa.ukitambua kuna mtu anamatatizo, shida , mitihani, fanya  haraka kuyatatua matatizo yake, kwani mwenyezi mungu ana sema fanyeni haraka kutaka msamaha wa mwenyezi mungu.”