Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq pamoja na Waumini wakiwa makini kusikiliza historia ya Jafar Ibn Abu Twalib.
Katika
Vita Vya Mu’utah Jafar ibn Abi Talib, kaka yake mkubwa Ali. Alipigana kishujaa
na kwa muda mrefu, akiwaua maadui wengi kiasi kwamba miili yao ilijipanga kama
kamba ya kuni kumzunguka yeye.
Lakini baadae askari wa Kirumi alitambaa kutoka nyuma,
bila ya kuonekana, na akampiga kwa upanga wake kwenye mkono wake wa kulia, na
akaukata kabisa.
Jafar hakuiachia bendera ianguke chini, na alizidi
kumbana adui.
Baadae kidogo, Mrumi mwingine akaja kutokea nyuma, na kwa pigo la upanga wake,
akaukata mkono wa kushoto pia.
Shujaa huyu, akiwa bado hajakata tamaa, aliishikilia
bendera chini ya kidevu chake, na akaendelea kusonga mbele.
. |