Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi amewataka Waislam kuwa wamoja ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbali zinazoukabili umma wa Kiislam.
Sheikh Zuberi amesema hayo jana kwenye Sherehe ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), iliyoandaliwa na Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania.
Katika Maulid hiyo Viongozi mbalimbali hususan kutoka Baraza kuu la Waislam Tanzania Wajumbe wa baraza hilo na Masheikh wa baraza hilo wa Mkoa wa Dar es salamm walihudhuria.
Ujio wa Mufti Zubery kushiriki katika
sherehe za Maulidi ya Mtume tena kwa dhehebu ambalo awali ilikuwa ni
vigumu kuhudhuria inaelezwa ni ishara tosha kuwa Kiongozi huyo
amedhamiria kuondoa ubagauzi uliopo kati ya kundi moja na lingine ambayo
yote yanasema yanamfuata Mtume Muhammad.