Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber |
Jamii imetakiwa kuwakemea watu wenye fikra ya kupotosha ili nchi iendelee kuwa na amani ,utulivu na mshikamano.
Akizungumza
jijini Dar es salaam Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari
Zuber,amesema kuna baadhi ya watu wanatumia mikusanyiko vibaya katika
kupotosha umma hivyo ni busara kila mtanzania kukemea kwa nguvu zote.
Amesema jamii inatakiwa kujenga mahaba na nchi yao ili kuepusha migogoro na uvunjifu wa amani usio wa lazima.
“jamii ikijenga mahaba ya dhati itasaidia nchi kuwa sarama na watu kufanya kazi zao kwa amani na utulivu “
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es alaam akiongea kwenye hafla ya futar hiyo. |
Naye
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa amesema kila
mmoja wetu aijenge nchi kwa kumtanguliza mungu na kuliombea.
“kujenga nchi yenye amani ni jukumu la kila mtanzania kwani amani ni
kimbilio la kila binadamu na ndo maana kila kwenye machafuko maendeleo
huwa duni tofautfi na nchi zenye amani”
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es salaamPadri JOHN SOLOMON akiongea kwenye hafla ya Futari hiyo |
Kwa upande wake Padri JOHN SOLOMON ,amesema amani ndiyo inaleta maendeleo endelevu katika nchi yeyote duniani.
“amani ni tunu aliyotupa mwenyezi mungu hivyo ni busala kila kiongozi
kuitngaza kwa nguvu zake zote zote ili matunda haya yawe kwa vizazi
vyetu”.
No comments:
Post a Comment