Friday, October 30, 2015

ACT Wazlendo Mama Anna Mghwira amtumia salamu za pongezi Dr. Magufuli

Mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea salamu za pongezi kutoka kwa mgombea Urais Mwanamke Pekee kwa tiketi ya ACT Wazlendo Mama Anna Mghwira.

 Mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza rasmi  matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam.

ambako yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni. Dkt Magufuli amemshukur sana Mama Mghwira na kumwita mkomavu wa siasa na mwana-Demokrasia wa mfano jioni hii Oktoba 29, 2015

Jaji Damian Lubuva Amtangaza Dr. John Pombe Mgufuli Kuwa Raisi Mteule wa Kiti cha Uraisi Tanzania

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akifafanua baadhi ya mambo mapema leo jioni  kabla ya mawakala wa vyama kusaini fomu namba 27 iliyosainiwa na mawakala wa vyama vya siasa .
 
Baada ya majumuisho ya kura kwa wagombea urais kabla ya kutangaza rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo Dk. John Pombe Magufuli ametangazwa mshindi kwa kura  kura 8.882.935 sawa na asilimia 58.46 

huku mpinzania wake kutoka Umoja wa Vyama vya  Upinzani kupitia chama cha Chadema Edwald Lowasa akipata kura 6.072.848 sawa na asilimia 39.97

Israel yauwa Wapalestina wawili Ukingo wa Magharibi

Wanajeshi wa Israel leo wamewauwa Wapalestina wengine wawili katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kuwapiga risasi. 

Mauaji hayo ni katika mlolongo wa mashambulizi yanayoendelea kufanywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na katika mwezi huu pekee utawala huo umewauwa shahidi makumi ya raia wa Palestina wasio na hatia yoyote.

Mpalestina mmoja ambaye umri na utambulisho wake haujajulikana aliuawa shahidi leo karibu na mji wa al Khalil baada ya Israel kudai kuwa alitaka kumpiga kisu mwanajeshi mmoja. 

Watu walioshuhudia wamesema kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walimpiga risasi begani na kichwani Mpalestina huyo kwa mara kadhaa. 

Baadaye wanajeshi wa Israel walimuuwa kwa kumpiga risasi Mpalestina mwingine wamedai kuwa, alikuwa na lengo la kumchoma kisu mwanajeshi wa Israel. 

Hata hivyo mwanaharakti wa Kipalestina, Issa Amru, ambaye alikuwepo eneo la tukio amepinga madai hayo ya Israel na kusema kuwa Mpalestina huyo hakuwa na kisu.chanzo irib