Thursday, August 11, 2016

LIGI KUU TANZANIA BARA-RATIBA YABADILISHWA TENA LEO

Kutokana na sababu mbalimbali, Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imelazimika kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa michezo kadhaa ya mwanzo kama ifuatavyo.
1. Mchezo Na. 2 - Kagera Sugar vs Mbeya City (20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 21.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Sababu ni kuwa uwanja wa Kaitaba bado utakuwa kwenye matengenezo.
 2. Mchezo Na.4 - Toto African vs Mwadui FC (20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 24.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za mabadiliko ni kuwa uwanja huo tarehe 20.08.2016 utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.
3. Mchezo Na.13 - Kagera Sugar vs Stand United (27.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo huo ilikuwa ni Kagera Sugar, lakini kwa sasa timu mwenyeji atakuwa ni Stand United.
4. Mchezo Na.55 - Toto vs Ndanda (02.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 03.10.2016 badala ya tarehe 02.10.2016
5. Mchezo Na.80 - Mbao FC vs Ndanda fc (16.10.2016)
Mchezo huo umerudishwa nyuma kutoka tarehe 16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni kuiwezesha timu ya Ndanda kucheza michezo miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza gharama.
6. Mchezo Na.96 - Tanzania Prisons vs Mbao FC (22.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 23.10.2016 badala ya 22.10.2016 ili kuipa nafasi timu ya Mbao kupumzika na kusafiri. Tayari timu za Ligi Kuu ya Vodacom zimearifiwa na kuagizwa kuzingatia mabadiliko hayo.

"Madai kuwa Iran imeipa Daesh silaha ni kichekesho"

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha madai ya kipropaganda yanayoenezwa na vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa Tehran imelipa silaha kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kuwa, madai hayo ya Wazayuni kwamba silaha za nchi hii zimepatikana mikokoni wa Daesh katika Peninsula ya Sinai nchini Misri hayana msingi na yametolewa kwa nia ya kuficha ukweli wa mambo kuhusu uhusiano wa utawala huo bandia na matakfiri wa Daesh. 

Uhusiano wa karibu wa Daesh, Saudia na Israel
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, dunia imezinduka na kila mmoja anafahamu kuwa, kundi la kigadi na kitakfiri la Daesh linapokea misaada ya moja kwa moja kutoka nchi za Magharibi na utawala haramu wa Israel, ikiwemo misaada ya kifedha na silaha.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imesisitiza kuwa, sera na misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya makundi ya kigaidi yakiongozwa na Daesh iko wazi na daima taifa hili limekuwa mbioni kukabiliana na harakati za kigaidi.

Wanachama wa Daesh katika eneo la Sinai, Misri
Kadhalika taarifa hiyo imeongeza kuwa, dunia nzima sasa inafahamu uhusiano kati ya Daesh, utawala wa Kizayuni, Marekani na Saudi Arabia na kwamba ni wazi sasa walimwengu wanajua kundi hilo la wakufurishaji lilibuniwa ili kuzusha hofu, kuvuruga amani na kusababisha ukosefu wa usalama na uthabiti sio tu katika eneo hili bali kote duniani.Miezi kadhaa iliyopita, jeshi la Misri lilianzisha operesheni kubwa katika maeneo ya Rafah, Sheikh Zuweid na al Aris huko Sinai Kaskazini kwa lengo la kuyatokomeza magenge hayo ya kigaidi.Chanzo.parstoday