Monday, June 8, 2015

Maalim Seif Ni Mwisho Wa Matatizo



SHUGHULI mbalimbali zilisimama kwa muda wakati wa mkutono wa Chama cha Wananchi (CUF) uliohutubiwa na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad. Anaandika Mwandishi Wetu Zanzibar … (endelea).
      Maalimu Seif ambaye tayari amechukua fomu kugombea urais kupitia chama hicho, alihutubia maelfu ya wananchi na wakazi wa Zainzibar kwenye Uwanja wa Kibandamaiti, visiwani humo. 
       Hali ilivyokuwa, wakazi wengi wanaoishi karibu na uwanja huo walisimamisha shughuli zao na kuungana na wananchi kutoka maeneo mbalimbali visiwani humo ili kuhudhuria mkutanmo huo.
Katika mkutano huo, Maalim Seif aliwaahidi Wazanzibar kubadilisha kisiwa hicho na kuwa kisiwa chenye matumaini na fursa mbalimbali za kiuchumi tofauti na ilivyo sasa chini ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
“Nakusudia kuifanya Zanzibar kuwa visiwa vya fursa za biashara na ajira kwa wananchi.”
Maalim Seif ambaye tayari chama chake kimemteua rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya urais visiwani humo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.
Amesema, Zanzibar inazo fursa nyingi za kuweza kunyanyua kipato cha wananchi, na kwamba ataweka kipaumbele katika kuziibua na kuziendeleza fursa hizo.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katika kujenga mazingira bora ya uwekezaji, ataisimamia ipasavyo Mamlaka ya vitega uchumi, ili kuondosha vizingiti vinavyokwamisha uwekezaji nchini.
Amefahamisha kuwa wapo wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kuwekeza miradi mikubwa ya kiuchumi, lakini wamekuwa wakipata usumbufu, jambo ambalo ameahidi kulishughulikia muda mfupi baada ya kuingia madarakani.
Sambamba na hilo, Maalim Seif amesema iwapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar, atahakikisha kuwa Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, ili kurahisisha shughuli za kibiashara ikiwemo Utalii.
Amesema hatua hiyo itakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma za viwanja vya ndege, ambavyo vitaweza kutoa huduma bora kitaifa na kimataifa.
Aidha amesema chini ya uongozi wake iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ataitangaza Zanzibar kuwa bandari huru, sambamba na kujenga bandari mpya itakayotoa huduma bora kwa mwambao wa Afrika Mashariki.
Katika hatua nyengine Maalim Seif amesema anakusudia kuongeza viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wote, pamoja na kuzingatia maslahi ya wastaafu na wazee wasiojiweza.
Akizungumzia kuhusu mafuta, Maalim Seif amesema anakusudia kuanzisha Wizara ya Mafuta na Gesi ili kurahisisha uchimbaji wa nishati hiyo, itakayoondosha hali ya umasikini katika visiwa vya Zanzibar.
Maalim Seif pia alizungumzia hali ya amani na utulivu nchini, na kueleza kuwa amani ya kweli itapatikana iwapo vyombo vinavyohusika vitatoa haki kwa wananchi wote.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeshawika kumuidhinisha Maalim Seif kuwa mgombea Urais wa Zanzibar, kutokana na uwezo na nia ya dhati ya kuwatumikia wazanzibari.
Amesema, viongozi waliopo madarakani wana dhamana na wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unafanyika katika hali ya amani, sambamba na kuheshimu maamuzi ya wananchi katika uchaguzi huo.

Kumbukumbu ya Imam Khomein (r.a) yafanyika nchini Tanzania



Waumini wa dini ya Kiislam wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah pamoja na Waislam Madhehebu ya Sunni wameshirikiana kwa pamoja kufanya kumbukumbu ya Imam Khomein (r.a) ambaye hivi sasa ametimiza miaka 26 tangu kifo chake.
Kumbukumbu ilifanyika katika ukumbi wa Khojja Shia Ithna Ashariyyah uliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Mgeni rasmi alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum.

Imam Khomein (r.a) alifariki dunia Saa nne na dakika ishirini siku ya Jumamosi usiku sawa na tarehe 3/06/1989, ikiwa ni baada ya kukaa hospitali muda wa siku kumi.

Ilipofika tarehe tano mwezi wa sita uliwekwa mwili wake uliyotakasika kwenye kiwanja kikubwa cha kusalia cha jiji la Tehran ili Umma wa Wairani uweze kumuaga. Kisha mwili wake uliyotakasikia ulisindikizwa 
Na msafara wa watu zaidi ya Milioni kumi wakiwa wamevaa na kujifunika mavazi meusi huku wakimwaga machozi na kutoa sauti ya kuishiwa nguvu kutokana na hasara waliyoipata ya kuondokewa na mtu mkubwa na kiongozi shupavu.
Waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu kutoka katika madhehebu mbalimbali hapa nchini

Wawakilishi wa vyombo vya habari walishindwa kuuelezea vilivyo au kuutolea picha halisi msafara huo wa mazishi, kwani ulikuwa ni msafara wenye urefu wa kilometa kumi na saba. Lakini wawakilishi wa vyombo vya habari vya Magharibi bila hiyari yao wakaelezea msafara huo wa mazishi kwa kusema: "Ulikuwa wa kipekee kwa ukubwa, na ni msafara ambao haujawahi kupatikana mfano wake ulimwenguni."

Imam Khomein (r.a) alizikwa pembezoni mwa makaburi ya Mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislam, kwenye moja ya kona za makaburi ya Zahraa mjini Tehran. Maombolezo yalienea kona zote za Iran na kwa Waislam wengine wote ulimwenguni kwa muda wa siku Arobaini huku sehemu zote zikiwa zimeenea bendera nyeusi na kuenea vikao vya Maombolezo ya kumpoteza mtetezi wa heshima ya Uislam.
Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wakiimba qaswida ya maombolezi ya kumkumbuka imam Khomein (r.a)

Na sasa kaburi lake limekuwa ni sehemu na kituo cha ziara kwa kila siku kutembelewa na Waislam na watu huru kutoka kona zote Ulimwenguni."Nijukumu la kila mmoja wetu kufuata nyayo za kiongozi huyu shupavu na wa heshima."Tusikae kimya katika maisha yetu pindi tunapoona dhulma inafanyika katika jamii zetu