Monday, June 8, 2015

Kumbukumbu ya Imam Khomein (r.a) yafanyika nchini Tanzania



Waumini wa dini ya Kiislam wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah pamoja na Waislam Madhehebu ya Sunni wameshirikiana kwa pamoja kufanya kumbukumbu ya Imam Khomein (r.a) ambaye hivi sasa ametimiza miaka 26 tangu kifo chake.
Kumbukumbu ilifanyika katika ukumbi wa Khojja Shia Ithna Ashariyyah uliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Mgeni rasmi alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum.

Imam Khomein (r.a) alifariki dunia Saa nne na dakika ishirini siku ya Jumamosi usiku sawa na tarehe 3/06/1989, ikiwa ni baada ya kukaa hospitali muda wa siku kumi.

Ilipofika tarehe tano mwezi wa sita uliwekwa mwili wake uliyotakasika kwenye kiwanja kikubwa cha kusalia cha jiji la Tehran ili Umma wa Wairani uweze kumuaga. Kisha mwili wake uliyotakasikia ulisindikizwa 
Na msafara wa watu zaidi ya Milioni kumi wakiwa wamevaa na kujifunika mavazi meusi huku wakimwaga machozi na kutoa sauti ya kuishiwa nguvu kutokana na hasara waliyoipata ya kuondokewa na mtu mkubwa na kiongozi shupavu.
Waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu kutoka katika madhehebu mbalimbali hapa nchini

Wawakilishi wa vyombo vya habari walishindwa kuuelezea vilivyo au kuutolea picha halisi msafara huo wa mazishi, kwani ulikuwa ni msafara wenye urefu wa kilometa kumi na saba. Lakini wawakilishi wa vyombo vya habari vya Magharibi bila hiyari yao wakaelezea msafara huo wa mazishi kwa kusema: "Ulikuwa wa kipekee kwa ukubwa, na ni msafara ambao haujawahi kupatikana mfano wake ulimwenguni."

Imam Khomein (r.a) alizikwa pembezoni mwa makaburi ya Mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislam, kwenye moja ya kona za makaburi ya Zahraa mjini Tehran. Maombolezo yalienea kona zote za Iran na kwa Waislam wengine wote ulimwenguni kwa muda wa siku Arobaini huku sehemu zote zikiwa zimeenea bendera nyeusi na kuenea vikao vya Maombolezo ya kumpoteza mtetezi wa heshima ya Uislam.
Wanafunzi wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) wakiimba qaswida ya maombolezi ya kumkumbuka imam Khomein (r.a)

Na sasa kaburi lake limekuwa ni sehemu na kituo cha ziara kwa kila siku kutembelewa na Waislam na watu huru kutoka kona zote Ulimwenguni."Nijukumu la kila mmoja wetu kufuata nyayo za kiongozi huyu shupavu na wa heshima."Tusikae kimya katika maisha yetu pindi tunapoona dhulma inafanyika katika jamii zetu

No comments: