Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah |
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kuna udharura mkubwa wa kutumiwa vyema siku hizi za maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika mwezi huu wa Muharram na kuwataka viongozi wa Lebanon kuwa makini katika kuzima njama zilizopangwa za kuzusha fitina na mifarakano kaskazini mwa nchi hiyo.
Akizungumza
kwa mnasaba wa kuanza mwezi wa Muharram na kukumbuka masaibu ya kuuawa shahidi
Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake watiifu katika ardhi ya Karbala.
Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea matukio
mbalimbali katika nyanja za kisiasa, kiusalama, kifikra, kidini, kiuchumi
kiimani na kijamii na kusisitiza kwamba, leo hii umma wa Kiislamu unapaswa kuwa
macho katika kukabiliana na changamoto kubwa ya makundi ya kitakfiri na kigaidi
katika eneo la Mashariki ya Kati na hasa katika nchi za Lebanon, Iraq na Syria.
Sayyid Nasrullah amelielezea tukio la Karbala na
kusisitiza kwamba, tukio hilo litaendelea kubaki katika historia ya mwanadamu
kwani limepelekea kuhifadhiwa Uislamu na watu wote wanajukumu la kubainisha
kilichojiri katika ardhi ya Karbala.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa, watu
wanaofikiri kwamba kwa kuanzisha vita vya kisaikolojia na vitisho wataweza
kuzuia kufanyika maombolezo ya Aba Abdillah Imam Hussein AS wanajidanganya,
kwani vitisho hivyo havitawatenganisha na Imam Hussein AS.
http://kiswahili.irib.ir/habari/mashariki-ya-kati/item/44010-nasrullah-vitisho-havitazuia-maombolezo-ya-imam-hussein-as