Wanafunzi na Wanahakati wa Imam Jaafar Swadiq wakisafisha makaburi. |
Sheikh Salim Mwamba wa Hawza ya Imam Jafar Swadiq akisafisha makaburi ya Kintinku,kidogo dar es salaam. |
Habari Kamili
Hawza ya Imam Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala imewataka
Wananchi pamoja na Serikali kusimamisha Haki na kuifanyia kazi haki ili kupata
jamii bora.
Hayo ameyasemwa Sheikh Salim Mwamba wakati Wakifanya Usafi katika
Makaburi yaliyopo Kintiku, Kigogo, Jijini Dar es salaam, wakikumbuka kifo cha
Mjukuu wa Mtume Imam Hussein (a.s).
“Imam Hussein (a.s) alitoka Makka akaenda Iraq kwa ajili ya
kusimamisha haki aliyosimamisha Babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuwataka
watu waitekeleze haki”alisema Sheikh Mwamba.
Sheikh Mwamba ameongeza kuwa Jamii na Serikali wanatakiwa kutoa
haki kwa usawa bila ya kuegemea katika udugu, ujirani wala udini, ili kujenga
jamii yenye kupenda Haki.
“Jamii na Serikali ikitoa haki kwa usawa bila kuegemea upande
wowote, itajenga jamii yenye kupenda haki na kuisimamia haki kama
alivyoisimamia Imam Hussein ( a.s) mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w),
aliongeza Sheikh Mwamba.
Waislamu kote ulimwenguni huadhimisha mwezi huu kwa huzuni kubwa
kwa kukumbuka kifo cha Imam Husain (a.s.), mjukuu wa Mtukufu Mtume Muhammad
(s.a.w.w.).
Imam Hussein (a.s) alizaliwa na Fatma bint wa Mtukufu Mtume
Muhammad (s.a.w.w) na Amirul Muuminina Ally tarehe 15, mwezi wa Shaaban Mwaka 4
A.H na aliuwawa tarehe 10 Muharram katika mji wa karbala nchini Iraq.
No comments:
Post a Comment