Monday, September 21, 2015

Moto Waunguza Sehemu Ya Mlima Meru



HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
New Picture (2)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MOTO WAUNGUZA SEHEMU YA MLIMA MERU
Moto mkubwa umezuka mwishoni mwa wiki hii na kuunguza sehemu ya Mlima Meru katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo cha moto huo ni vitendo haramu vya urinaji wa asali ndani ya msitu wa hifadhi hiyo.
Wananchi wapatao 200 kutoka vijiji jirani vya Olosinoni na Kisimiri Juu wakishirikiana na TANAPA wamefanikiwa kuudhibiti moto huo ili usiweze kuleta madhara makubwa kwa binadamu hususan wageni wanaotembelea hifadhi kwa lengo la kupanda Mlima Meru.
Hadi sasa hakuna wageni waliodhurika na moto huo na tahadhari zote zimechukuliwa ili kudhibiti madhara zaidi kwa binadamu na shughuli za utalii ndani ya hifadhi.
Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea kuwatahadharisha wananchi juu ya vitendo vya kuingia ndani ya hifadhi bila kibali kwa shughuli ambazo zinaweza kuwa chanzo cha kuzuka kwa mioto hii ambayo husababisha uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibu vyanzo vya maji.
Aidha, katika kuhakikisha kuwa moto huo unadhibitiwa kwa haraka, TANAPA imeongeza nguvu kazi ya wananchi wakishirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuweza kuudhibiti moto huo.
Mwisho, taarifa kamili juu madhara yaliyosababishwa na moto huo itatolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuzima moto na umma utaendelea kupewa taarifa ya maendeleo ya zoezi la uzimaji wa moto kila wakati.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA 21.09.2015 dg@tanzaniaparks.com www.tanzaniaparks.com.
chanzo-fullshagwe

Kenyatta: 'Hatuwezi kulipa walimu'

Wakati shule zote za umma na binafsi zikianza kufungwa kuanzia hii leo nchini Kenya, Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo. (Hotuba yake kamili ipate hapa, Kenyatta: Hatuwezi kuwalipa walimu)
Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.
Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT ameambia BBC kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.
Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule "zamani". Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenza.chanzo bbc-swahili

Shule zafungwa Kenya kutokana na mgomo wa Walimu

Wanafunzi wengi Kenya wamelazimika kusalia nyumbani baada ya serikali kuagiza kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi leo kutokana na mgomo wa walimu.
Ingawa shule za umma zimefungwa, baadhi ya shule za kibinafsi zimekaidi agizo la serikali na kuendelea na masomo.
Chama cha shule za kibinafsi kimesema kitawasilisha kesi mahakamani leo kupinga agizo hilo la serikali lililotolewa na Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi Ijumaa wiki iliyopita.
Wazazi wanaowapeleka watoto wao katika shule za kibinafsi, nyingi ambazo hutoza karo ya juu, wametoa hisia kali kutokana na tangazo hilo wakishangaa ni kwa nini shule hizo zinafungwa.
Katika shule za umma, ni watahiniwa wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa waliosalia shuleni.
Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) kuna watahiniwa 937,467 wanaojiandaa kufanya mtihani wa darasa la nane KCPE utakaoanza Novemba 10 na kumalizika Novemba 12.
Watahiniwa wanaojiandaa kufanya mtihani wa kidato cha nne KCSE utakaoanza rasmi Oktoba 12 ni 525,802.
Baraza hilo limesema mitihani hiyo haitaahirishwa.
Kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga, Rais Uhuru Kenyatta na baadaye kutumwa kwa vyombo vya habari alisema haiwezekani kwa walimu kuongezewa mishahara na kuwataka warejee kazini.
Mahakama ya Juu Kenya iliitaka serikali kutii agizo la mahakama ya rufaa iliyoitaka serikali kutii uamuzi wa mahakama ya kiviwanda na kuwalipa walimu nyongeza ya asilimia 50 hadi 60.
Serikali kupitia Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) imepinga agizo hilo.
Mahakama ya Viwanda inatarajiwa kutoa uamuzi Ijumaa wiki hii kuhusu iwapo mgomo huo wa walimu, uliotatiza masomo Kenya tangu zifunguliwe kwa muhula wa tatu, ni halali au la. chanzo bbc-swahili

Mabasi 138 ya Mwendo Kasi Yaingia Nchini


TATIZO la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linatarajia kupungua kufuatia kuanza kupindi cha mpito cha mabasi Yaendayo Haraka (BRT) mwezi ujao kufuatia kuwasili kwa mabasi 138 katika Bandari ya Dar es Salaam kutoa China tayari kwa huduma ya usafiri. 
Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki aliwaambia waandishi wa habari jana wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa mabasi hayo, kuwa wakazi wa Dar es Salaama kwa sasa wataanza kutumia usafiri wa mabasi hayo. 
“Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito," hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili", alisema na kuongezeas kuwa kampuni hiyo imepewa jukumu la kuendesha kipindi cha mpito ili waweze kupata uzoefu na zabuni ya mwendesha mradi kipindi cha kudumu itakapo tangazwa itasaidia wao kushindana. 
 Alisema serikali ilifanya kazi kubwa kuwainganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya UDA-RT. 
Aidha alikanusha kuwa nauli za mabasi hayo imepangwa kuwa Tsh. 900 zilizotolewa katika mitandao ya jamii, nakusema huo ni uzushi na upotoshaji na aliyefanya hivyo anatafutwa ili sheria ichukue mkondo. 
Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia. 
Msemaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit(UDA-RT),Bw,Subri Maburuki alisema mabasi yote yameingia yakiwemo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mipito itanza baada ya kukamlisha taratibu za bandari. 
 “Tuliahidi kuwa mwezi huu wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni keli yamemekuja,” na kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa jumla mabasi 140", alisema Bw. Maburuki na kufafanua kwamba mabasi hayo yametokea kiwandani China na yanakidhi miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana. 
Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Hebel Mhanga alisema meli iliyobeba mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi ilitokea China ilikuwa imebeba magari 1700 yakiwemo mabasi ya UDA-RT. 
“Hatua hii ni ya msingi kwa nchi yetu, itasaidia wakazi kusafiri kwa urahisi na haraka,”alisema Bw. Mhanga.
UDA-RT ni kampuni iliyoundwa na wazalendo kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya DART jijini Dar es Salaam.chanzo fullhabari

Wanamgambo 75 waliofunzwa na US waingia Syria

Makumi ya wanamgambo ambao wampatiwa upya mafunzi na muungano wa Marekani unaodai kupambana na matakfiri wa kundi la Daesh wameingia nchini Syria wakitokea Uturuki. 
Shirika la Haki za Binadamu la Syria(SOHR) limeripoti kuwa wanamgambo 75 wameingia kaskazini mwa Syria siku chache zilizopita wakiwa kwenye msafara wa makumi ya magari yenye silaha nyepesi na zinginezo. 
Rami Andulrahman Mkurugenzi wa shirika hilo la haki za binadamu la Syria amesema kuwa wanamgambo hao waliopewa mafunzo kwenye kambi moja karibu na mji mkuu wa Syria wailiwasili katika mji wa Aleppo nchini Syria kati ya juzi isuki na jana asubuhi.
Mpango huo wa kutoa mafunzo kwa makundi ya wanamgambo unaoongozwa na Marekani nchini Uturuki, uliasisiwa mwezi Mei mwaka huu lengo likiwa ni kuwapa mafunzo wanamgambo 5400 wanaotajwa kuwa wenye misimamo ya wastani ili kutekeleza kile kinachotajwa na Washington kuwa ni vita dhidi ya kundi la Daesh huko Syria.  
Mwezi uliopita, Walid al Muallem Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria aliilaumu Marekani kwa hatua yake ya kutofautisha makundi ya kitakfiri yanayopigana dhidi ya serikali ya Damascus na kusema kuwa, Kwa wao  huko Syria, hakuna kitu kama hicho eti wapinzani wenye misimamo ya wastani na kinyume chake na kwamba yoyote anayebeba silaha dhidi ya serikali ya Syria ni gaidi. 

HAMAS yanasa droni nyengine ya Israel, Gaza

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema imeinasa ndege isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ikiwa ni droni ya pili kunaswa na harakati hiyo ya muqawama katika kipindi cha miezi miwili. 
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa wanamapambano wa tawi la kijeshi la Hamas Izzuddin al-Qassam waliikamata droni hiyo baada ya kuanguka katika eneo la Beit Lahia kaskazini mwa Gaza. 
Mnamo mwezi Julai, harakati wa muqawama ya Hamas ilitangaza kuwa droni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeangukia huko kaskazini mwa Gaza na kuongeza kuwa wanamapambano wa harakati hiyo wamefanikiwa kuitengeneza ndege hiyo isiyo na rubani. 
Utawala wa Kizayuni umekuwa ukizitumia mara kwa mara ndege zisizo na rubani kukusanyia taarifa za kijasusi katika eneo la Ukanda wa Gaza ambalo limewekewa mzingiro wa kidhalimu wa kijeshi na kiuchumi na utawala huo ghasibu tangu mwaka 2007. 
Tokea mwaka 2008 hadi sasa utawala wa Kizayuni umeshaishambulia kijeshi Gaza mara tatu, ambapo katika vita vya siku 50 vya mwaka uliopita Wapalestina wasiopungua 2,140 wakiwemo watoto 557 waliuliwa shahidi, mbali na 11,100 waliojeruhiwa na wengine 170,000 waliobaki bila makaazi.CHANZO IRB

Angalia Picha 9 za Dk. John Pombe Magufuli akiwa wilayani CHATO

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wake wa kampeni kwenye uwanja wa Chato wialayani Chato mkoani Geita ambapo amewaomba wananchi wa Chato ambako ndiko alikozaliwa kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Dk. Magufuli amesema mara atakapochaguliwa serikali yake itakuwa ni ya Watazania wote bila kujali vyama vyao, Dini zao, Makabila yao wala Itikadi zao atakuwa rais wa watanzania wote na lengo lake kubwa ni kuwatumikia watanzania na kuangalia zaidi na kuboresha hali za watanzania masikini ili nao waweze kukua kiuchumi.
Dk. Magufuli amesema kuna watu wameanza kuwatisha wananchi kwamba yeye ni mkali, Amesema “Si kweli yeye ni mpole sana ila nikiwa madarakani  nitaongoza nchi kwa utawala wa sheria na kuwapa haki watanzania  kulingana na sheria za nchi zanavyoelekeza kuendesha nchi hivyo sitakuwa kiongozi dikteta kama wanavyofikiri wengine”.  Japokuwa ninauchukia uzembe kazini, Wizi  na ufisadi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-CHATO)