Monday, October 2, 2017

Matembezi ya Amani ya Siku ya Ashura -Dar es salaam-Tanzania

Mabadiliko aliyoyaleta Imam Hussein (a.s) ambayo alikubali kuuwawa yeye pamoja na kizazi chake,pamoja na watoto wake pamoja na wanawake aliokuwa nao, msiba huo mkubwa uliomkumba kwaababu ya kuleta mabadilko, 

Mabadiliko hayo makubwa yalikuwa ni kuiteneneza jamii,jamii aliyoihi ilikuwa ni jamii iliyokuwa na mapungufu mengi mno akatoka na akakubali yeye auwawa pamoja na wanawe kwa ajili ya jamii ibadilike.katika mabadiliko makubwa aliyopambana nayo Imam Hussein(a.s) ni kuwa na mabadilioko ya umoja, 

Watu walikuwa wamepoteza kuwa kitu kimoja, Imamu husein (a.s) akakubali afe yeye na wanawe ili jamii alipokuwa anaishi ikamatane na kitu kinachoitwa umoja,na mimi naamini ya kwamba matembezi haya ya amani yaliyoko leo katika mkoa wa dare s salaam na ambayo yako katika nchi za wailamu husuani wailamu wa dhehebu la shia ithnasheriya.

Naamini ya kwamba matembezi haya yatakuwa ni chachuya kuwaleta watanzania waislamu kwanza kuwa kitu kimoja wenyewe kwa wenyewe lakini pili matembezi hayo yatakuwa chachu ya watanzania  wote kuwa kitu kimoja. Imam Husein (a.s) katika mambo amabyo alitoka kwa ajili yake na akafa kwa ajili yake ilikuwa ni kutetea uwanadamu ni kutetea utu, 

Leo ninaamini yakwamba dunia inahitajia utu,leo naamini ya kwamba  si Tanzania tu bali mahala popote pale dunianai wanautafuta utu wa mwanadamu urudishwe, kwa hivyo naaminiya kwamba matembezi haya ya amani huzuni hii tuliyokuwa nayo itakuwa ni chachu kubwa mno katika ardhi ya Tanzania kuhakikisha utu unarudi katika ardhi ya watanzania,

Watanzania itakiuwa ni sababu ya husein huyu itakuwa sababu kubwa ya sisi kutokubaguana, itakuwa ni sababu kubwa ya sisi kupendana na kuelewana, kwahovyo ninaamini ya kwamba imam Hussein(a.s) anahitajika leo katika ardhi ya Tanzania , 
 Image may contain: 6 people
Imam Hussein (a.s) moja katika malengo yake na katika maelekezo yake makubwa mabadiliko yake makubwa ilikuwa ni amani iliyopotea wakati wake imesambaratika, Hussein akakubali yeye na watoto wake wadogo wauwawe wengine wenye chini ya umriwa miezi 6, 

kwanini kwa sababuya kuboresha amani , utulivu na maelewano kwa wakati ule.ninaaminiya kwamba dunia leo umegubikwa na machafuko, kila mahala vita, makundi ya magaidi naamini ya kwamba vilevile Tanzania nayo inauhitajia utulivu, inahitajia amani, na inahitajia mshikamano.

Naamini yakwamba matembezi haya ya amani leo yaliyotoka katika nchi hii ya Tanzania yatakuwa ni chachu ya kuboresha amani tuliyokuwa nayo  katika nchi ya tanzania matembezi haya ya amani yatakuwa ni chachu ya kuboresha umoja na mshikamano na mashirikiano yaliyoko kati watanzania amabao hawabaguani dini zao hawabaguani rangi zao hawabaguani kabila zaowatanzania wote wanakusanywa na lugha yao ya Kiswahili, wanapendana wanaelewana na wanashikamano, wakristo waislamu hawabaguani kwa dini zao, bali wanaheshimiana na kupendana, 

Naamini yakwamba matembezi haya yatazidi kuiboresha Tanzania kuwa kisiwa cha amani kuwa mji wa maelewano, kuwa taifa amabalo watu wake wanapigiwa mfano kwa kupendana na kwa kushirikiana na haya ni mafunzo tunayoyapata katika msafara wa imam Hussein (a.s) mjukuu wa mtume Muhammad (s.a.w.w). Poleni kwa msiba wa Imam Husein (a.s).

Na:Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania.
Matembezi ya Amani, Siku ya Ashura, 01/10/2017.
Kuanzia Ilala Boma hadi Kigogo, Dar e salaam.