Harakati ya hawza Imam Swadiq chini ya Uongozi wa Samahat Sheikh Hemedi
Jalala inaungana na Waislamu wote duniani na Wapenzi wa Amani kokote walipo
kupinga kwa Kauli thabiti hatua zozote zinazochukulia na Serikali za nchi za
Magharibi na Marekani kuchochea vitendo venye lengo la kuamsha chuki na
machafuko ya Kidini ulimwenguni.
Kauli hivyo imetolewa baada tu ya Jarida linalochapisha vibonzo mjini Paris nchini Ufaransa Charlie Hebdo lilisema katika toleo lake la hapo kesho siku ya Jumatano(14/01/2015) litachapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wa mbele, akiwa na bango lenye maandishi “Je suis Charlie”, ikimaanisha “mimi ni charlie nimesamehe yote”.
Aidha alisema kuwa vitendo hivi vinafanywa na makundi ya Watu waovu, Wasio na Imani ya Dini wala Ubinaadamu, wanaopata kinga ya kulindwa na ufadhili wa Idara za Kijasusi za Mataifa na dola za Magharibi kwa lengo lao ovu la kutaka kuupaka Matope Uislamu na Waislamu duniani. |
Samahat Sheikh.Hemed Jalala. |
“Kuheshimu Imani, Mila, Tamaduni na
Matukufu ya Imani za Dini tofauti tofauti ni kanuni ya Msingi ya Umoja wa
Kimataifa, tunawataka wakuu wa Dola za Magharibi na Amerika kuwa Vinara
kuziheshimu na kutekeleza kwa vitendo kanuni na Haki hizi”alisisitiza Jalala.
Alisema kuwa Maamuzi yasio ya Upendeleo wa kiimani na yenye Maslahi sawa kwa
raia wa Imani tofauti tofauti wa Mataifa yao. Kwani ni kwa Maamuzi
wanayoyafanya yenye upendeleo wa Makusudi kwa Upande mmoja wa Imani ya Dini na
kukandamiza upande mwingine ndio chanzo cha kuzuka makundi yenye misimamo
mikali na yenye mikakati ya kulipiza kisasi na kufanya vitendo vya Kigaidi.
“Wanatumia gharama kubwa kukandamiza maandamano ya Amani yanayoitishwa
katika nchi zao kulaani Vitendo viovu na vya kigaidi vinavyofanywa na Taifa
ghasibu la Israel? Sambamba na hili tunaungana na Ulimwengu mzima kupinga Vitendo vyovyote vya
kigaidi vinavyofanyika duniani kote dhidi ya Nchi na au binaadamu yeyote asiye
na hatia”alisema Jalala.
Jalala aliongeza kuwa Hakuna uhuru usio na Mipaka, Matumizi mabaya ya Vyombo
vya habari na Mawasiliano, Imani na Misimamo inayokiuka mipaka ya Dini na
Sheria za Nchi, Mauaji na Udhalilishaji wa Viongozi wenye kuheshimiwa wa Dini
na Nchi, Kukashifu na Kutakana Matukufu ya Dini na uvunjaji wa Alama za dini
zinazoheshiwa na waumini wa Dini hizo, ni Vitendo Viovu.