Kiongozi Mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari nje kidogo ya ukumbi wa Semina wa Threatre One University of Dar es salaam. |
Watanzania wametakiwa
kuhakikisha kuwa wanadumisha umoja, haki na Amani iliyopo nchini ikiwa ni pamoja na
kutenda mambo mema ili kuwaenzi kwa vitendo Immam Husein (a.s) na Masih Issa / Yesu (a.s) ambao
walipambana duniani kuhakikisha kuwa wanasimamia haki katika Dunia kwa ujumla.
Wito huo umetolewa Leo
Jijini Dar es salaam na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala wakati
wa semina maalum yenye anuani"Jitihada za Imam Hussein (a.s) na Masih Issa / Yesu (a.s) katika kueneza haki na amani Duniani.
Semina hiyo ikijadili kwa pamoja Jitihada za wawili
hao katika kuleta Amani na utulivu pamoja na kuleta haki na usawa
Duniani
ambapo Jalala amesema kuwa watu hao ni mfano wa kuigwa kwa sasa hii
ikiwa ni semina pia ya kuadhimisha Arobaini ya Mjukuu huyo wa Mtume
Muhamad (s.a.w.w).
Sheikh Jalala amesema
kuwa Semina hiyo inalengo la kuweka ulinganisho kwa watu hao wawili ambao ni
Imam Husein na Nabii Isaa ambaye ni Yesu ambao wote kwa pamoja walikuja Duniani
kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwenye Dunia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo
Haki kwa watu wote,na kutetea wanyoonge na kufanya watu wapendane katika Jamii.
Ameongeza kuwa ni
wakati wa watanzania kuacha mambo mambo mabaya na kuanza kufanya matendo ya
kiumpendaza mungu yakiwemo kupendana,kupinga dhuluma,na kutetea wanyonge ili
kuhakikisha kuwa wanawaenzi viongozi hao wa Kidini waliopambana kwa ajili ya
dunia.