Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema Sababu
kubwa inayowafanya Waislamu, hususani Waislamu Shia Ithnasheria Kutoka na
kufanya Matembezi ya Amani kuadhimisha
kifo cha mtume ni kuionyesha jamii huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na huruma kwa watu wote.
“Miaka zaidi
ya 1400 leo bado tunakumbuka Kifo cha Mtume Muhammd (s.a.w.w), kwanini tutoke
katika matembezi haya ya amani tunayoyaonyesha katika ardhi yetu ya Tanzania,
kwasababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitumwa kuwa na huruma kwa watu wote” Alisema
Sheikh Jalala.
Sheikh
Jalala alisema hayo mwiho wa wiki wakati wa matembezi ya Amani ya kukumbuka na
kuomboleza Kifo cha Mtume Mbora na mtukufu kwa watu wote ambae ni Muhammad
(s.a.w.w), katika matembezi yaliyoanzia Ilala Boma hadi Viwanja vya Pipo Kigogo
Dar es salaam.
“Siku ya
Kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni siku ya kukumbuka Utu,
Busara,Uwanadamu, kuwaheshimu wasiokuwa na Dini,kukaa vizuri pamoja na
Wakristo, Mayahudi, wanaoabudu Masanamu na Mapagani aliokuwa akiujali katika maisha yake”
aliongeza Sheikh Jalala.
Aidha Sheikh
Jalala alisema Mtume Muhammd (s.a.w.w) aliuwezi Waislamu kwa waislamu, Umoja wa
Watu wote na alitengeneza Umoja kati yake na Wakristo, Mapagani na Mayahud ,
umoja huu ulikkuwa ni wa kumsaidia mtu yoyote ambae atashambuliwa hatimae
akatengeneza Mazingira asiekuwa Mwislamu akishambuliwa Waislamu watanyanyuka
kumsaidia na Waislamu wakishambuliwa watu wa Dini nyingine na Madhehebu
nyingine watanyanyuka kuwasaidia
Waislamu.
“Napenda
kuwaelekeza Viongozi wa Kidini Masheikh, Maustadhi, Makasisi, Maskofu, na
Mashemas kwamba Mimbari au Madhabahu yao
Siku za Ijumaa au Siku za Jumamosi na Jumapili, Madarasa zao, Vyuo vyao
vitumike katika kuleta na kuboresha Amani ya watanzania wote, katika kuleta
maelewano, Mshikamano ya watanzania wote na Tiafa hili liendelee kuwa kisiwa
cha Amani” Alisisitiza Sheikh Jalala
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifariki Dunia tarehe 28, Mwezi wa Safar, Mwaka 11 Hijiria kwa Mujibu wa Kalenda ya Kiislamu, Mtume alikufa akiwa na Umri wa miaka 63.