Dar es Salaam. Muungano
wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umelitaka Jeshi la Polisi nchini
kubadilisha mtazamo na kuwaona waandishi wa habari kama wadau muhimu
kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza leo (Jumatano), wakati wa warsha maalumu ya kujadili usalama wa waandishi wa habari, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengulumwa amesema polisi hawana mwamko katika kuwalinda waandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao bali wao ndiyo wanaohatarisha usalama wao.
Amesema jeshi la polisi lina uwezo wa kulinda usalama wa waandishi wa habari lakini mwamko wao ni mdogo, hivyo wanahitaji kupata mafunzo maalumu ya kuwawezesha kubadili mtazamo wao juu ya tasnia ya habari.
"Tumeona katika nchi mbalimbali kwamba polisi hawawapendi waandishi wa habari. Hilo linatokana na mawazo hasi waliuonayo juu yao, tunahitaji kutoa elimu kwao ili watusaidie kuwalinda waandishi wanapotekeleza wajibu wao," amesema Olengulumwa.
No comments:
Post a Comment