Wednesday, November 2, 2016

Tanzania yashika nafasi ya pili utoaji huduma za kifedha

Dar es Salaam. Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa  kutoa huduma za kifedha kwa wateja wenye kipato cha kati na  cha chini.

Taarifa zilizotolewa na Shirikisho la Asasi za Huduma za kifedha Tanzania (Tamfi) zinaeleza kuwa kwa Tanzania huduma za kifedha zinawafikia wananchi 3,800,000.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari leo, Mwenyekiti wa Tamfi, Joel Mwakitalu alisema Tanzania imeshika nafasi ya pili kati ya nchi tano za Umoja wa Afrika Mashariki.
Nchi ambazo zilikusanywa taarifa ni kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.

Nchi ya kwanza imetajwa kuwa ni Kenya ambayo inawafikia watu milioni nne kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa mwaka 2014 katika nchi zote za EAC huku Tanzania zikisimamiwa na Shirikisho la Asasi za Huduma za kifedha Tanzania (Tamfi).


Mwakitalu alisema kinachosababisha huduma za kifedha  kutowafikia wateja wengi ni miundombinu kushindwa kuwafikia walio vijijini.

"Tumekutana na wenzetu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India kujadili ni namna gani huduma za kifedha zitawafikia wananchi wengi kupitia vikundi vidogovidogo kama Vicoba na vinginevyo kwakuwa vinawagusa sana wananchi wenye kipato kidogo," amesema Mwakitalu.

No comments: