Jaafar bin
Abu Talib (r.a), yeye alifanana naye Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa sura na
mwenendo. Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alimwambia:Jafar ibn Abu Talib “Umefanana na mimi kwa tabia na maumbile”.
Yeye ni Ja'far
ni mtoto wa tatu wa Abu Talib bin Abdul Muttalib na Fatima binti Asad, hivyo ni
binamu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ndugu zake wakubwa walikuwa Talib na Aqil;
ndugu zake wa kiume walikuwa Ali na Tulay
na dada zake walikuwa Fakhita, Jumana na Raita.
Wakati kulikuwa
na ukame hapo Makka, Abu Talib hakuweza kumudu kusaidia familia yake. Kwa hiyo
ndugu yake Abbas alichukua malipo ya vijana Ja'far. Ja'far alikuwa mfuasi wa
awali wa Uislamu. Mke wake ni Asma bint
Umays.
Wakati habari
kufikiwa Muhammad, alilia na kuomba kwa ajili ya nafsi Ja'far Yeye baadaye malaika Gabriel alishuka kuwafariji , akisema:
". Jafar alikuwa jasiri na waaminifu askari. Mungu amempa uzima wa milele,
na badala ya mikono yake ambayo kukatiwa katika vita, Bwana amempa jozi ya
mabawa (Atwayyar)
Hijra
ya mwanzo
Idadi ya Waislamu ilipoanza kuongezeka, na Makureshi
walipoanza kuwatesa Waislam na kuwafanyia kila aina ya vitimbi pamoja na kuwazuwia
wasifanye ibada zao ili wawarudishe katika dini yao ya kua
“Itakuwa bora kama baadhi yenu mtaondoka na
kuhamia nchi ya Uhabeshi, maana huko yuko mfalme ambaye hakubali mtu
kudhulumiwa ndani ya nchi yake, na ni nchi ya ukweli. Kwa hivyo hamieni huko
mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapoleta faraja Yake."
Wakaondoka Makka watu wapatao kumi wakiwemo Jaafar na mkewe
na Othman bin Affan na mkewe pamoja na Waislamu wengine na kuanza safari ndefu
ya kuhamia nchi ya Uhabeshi katika Hijra ya mwanzo. Kisha idadi yao ikaongezeka
na kufikia watu themanini na tatu, na walipowasili huko walipokelewa vizuri na
An Najashi mfalme wa Uhabeshi.
Katika Vita
vya Mu’uta majeshi mawili hayo moja likiwa na wapiganaji elfu tatu na lingine
likiwa na watu zaidi ya mia moja elfu, yakaanza mapambano makali sana na hatimaye
Zayd (r.a) akauliwa na kuanguka juu ya farasi wake.Wakafanya kama Mtume wa
Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alivyousia, Jaafar (r.a) akainyakuwa bendera kabla ya
kuanguka chini na akawa yeye ndiye anayeongoza mapigano hayo.
Vita vikali
vikaendela, na Warumi walipoona majeshi ya Kiislamu yaliyokuwa na idadi ndogo
ya watu kuliko wao yakipigana kwa ujasiri mkubwa, mkuu wa majeshi yao akatoa
amri kuwa mshika bendera lazima auliwe.
Warumi
wakaanza kuzielekeza nguvu zao zote kwa mshika bendera aliyekuwa Jaafar bin Abu
Talib, huku wakirusha mikuki na mishale kwa nguvu moja na kuwaelekeza
wapiganaji wao wakubwa wote upande wake, mpaka walipofanikiwa kumjeruhi na
kumuangusha kutoka juu ya farasi wake huku akiwa ameishika bendera kwa mkono
wake mmoja na huku akipigana kwa mkono wa pili.
Jaafar alimkata
miguu farasi wake kwa kuogopa asije akachukuliwa na Warumi na kumtumia katika
kuwashambulia Waislamu.Jaafar akawa anapigana akiwa anakwenda kwa miguu yake
bila ya farasi na kusonga mbele huku akiwakata makafiri vichwa vyao huku na
kule na huku akisoma mashairi ya kuisifia Pepo. Akawa anapigana nao mfano wa
jeshi la mtu mmoja mpaka alipokatwa mkono wake uliokuwa umebeba bendera.
Jaafar
akainyakuwa bendera kwa mkono wake wa pili na makafiri wakamzonga sana na
walipofanikiwa kumkata mkono wake wa pili, Jaafar akaikumbatia bendera kwa
mabega yake huku akiwa amesimama na na makafiri wakawa wanaendelea kumpiga kwa
panga zao mpaka alipokufa shahidi.
Anasema
Abdillahi bin Omar (Radhiya Llahu anhuma):
“Nilikuwa
pamoja na Jaafar katika vita vya Mu-utah, na baada ya kumalizika vita hivyo
tulimuona akiwa na majeraha ya panga na mikuki zaidi ya tisini, yote yakiwa
sehemu ya mbele ya mwili wake”.
Kadhalika mapokezi ya kauli ya Mtume (s.a.w.) na kukiri kwake juu ya kufaa
kulia kwa ajili ya wafu ni mengi. Mojawapo ni siku alipopata Shahada Bwana
Jaafar bin Abi Talib (At-Tayyaar), Mtume (s.a.w.w) alikwenda kwa mkewe (Jaafar)
Bibi Asmaa bint Umais ili kumpa faraja, naye Bibi Fatma aliingia pahala hapo
huku analia na kusema:
"Ewe Ami yangu". Basi Mtume (s.a.w.) akasema:
"Na walie wenye kulia kuwalilia mashujaa mfano wa Jaafar."
Imeandaliwa na
Twalha Zuberi Ndiholeye,
Kiongozi Mkuu wa Baqir Media.
Tarehe 19/03/2016, Sawa na 10,
Jamadal Akhir 1437.