Jaafar
akainyakuwa bendera kwa mkono wake wa pili na makafiri wakamzonga sana na
walipofanikiwa kumkata mkono wake wa pili, Jaafar akaikumbatia bendera kwa
mabega yake huku akiwa amesimama na na makafiri wakawa wanaendelea kumpiga kwa
panga zao mpaka alipokufa shahidi.
Anasema
Abdillahi bin Omar (Radhiya Llahu anhuma):
“Nilikuwa
pamoja na Jaafar katika vita vya Mu-utah, na baada ya kumalizika vita hivyo
tulimuona akiwa na majeraha ya panga na mikuki zaidi ya tisini, yote yakiwa
sehemu ya mbele ya mwili wake”.
Kadhalika mapokezi ya kauli ya Mtume (s.a.w.) na kukiri kwake juu ya kufaa
kulia kwa ajili ya wafu ni mengi. Mojawapo ni siku alipopata Shahada Bwana
Jaafar bin Abi Talib (At-Tayyaar), Mtume (s.a.w.w) alikwenda kwa mkewe (Jaafar)
Bibi Asmaa bint Umais ili kumpa faraja, naye Bibi Fatma aliingia pahala hapo
huku analia na kusema:
"Ewe Ami yangu". Basi Mtume (s.a.w.) akasema:
"Na walie wenye kulia kuwalilia mashujaa mfano wa Jaafar."
|
No comments:
Post a Comment