Wednesday, July 15, 2015

Sheikh Alhad Mussa aguswa na Siku ya Quds

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Alhad Mussa akitoa hotuba yake juu ya kulaani Uvamizi wa Kimabavu wa Wazayuni.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika semina maalum iliyoandaliwa na waislam wa dhehebu la shia kwa waialam pamoja na watu wote wanaopinga dhuluma na uonevu mbalimbali duniani,semina iliyofanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waumini wa dini ya kiislam pamoja na dini zote na wapinga uonevu wote.
Waumini wa Kike wakijitokeza kulaani uvamizi wa Wazayuni huko palestina katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya Quds

Wanaume nao wakiwa msitari wa mbele katika kuongoza matembezi ya amani ya kupinga Dhulma,unyanyasaji na Ukandamizaji unaofanyiwa watu wa palestina na Duniani Kote

Mabalozi kutoka nchi mbalimbali hapa Tanzania nao wakiwa pamoja na wananchi wa Tanzania katika kuwaunga Mkono suala la Siku ya Kimataifa ya Quds, katika Semina iliyofanyika Karimjee

Akizungumza katika semina hiyo mgeni rasmi ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa siku ya QUDS ni siku ya watu wote na madhehebu na dini zote na sio siku ya wapalestina pekee kwa sababu ni siku ambayo inatumika kupinga kwa sauti moja uonevu wowote ambao unaendelea katika mataifa mbalimbali duniani.
Amesema kuwa sisi kama Taifa la Tanzania ni siku muhimu ya kutafakari amani ya dunia ikiwa ni pamoja na kupinga kwa sauti moja dhuluma yoyote inayoendelea dhidi ya watu wa palestina na mataifa mengine duniani.
Waumini hao wameanza kuadhimisha siku hiyo jana ambapo walifanya matembezi ya amani katika jiji La Dar es salaam kuwakumbusha watanzania juu ya kuiombea na kuisaidia nchi ya pelestina kutoka katika machafuko ambayo yanazidi kugharimu maisha ya watu