Bi Grace Mugabe mke wa Rais Robert Mugabe wa
Zimbabwe ametumbukia katika sakata la ardhi baada ya kuzihamisha kwa nguvu
familia zaidi ya 200 katika makazi yao bila ya kuzipatia makazi mbadala.
Grace Mugabe aliwaamuru maafisa polisi waliokuwa
wamejizatiti kwa silaha, kuziondowa kwa nguvu familia hizo katika eneo lao la
mashamba ya Anold wilayani Mazowe mashariki mwa Harare mji mkuu wa Zimbabwe
bila ya kuwapatia sehemu nyingine ya kuishi katika kipindi hiki ambapo mvua
nyingi zinaonyesha.
Mkulima mmoja ambaye hakutaka kujulikana alisema kuwa baada ya polisi kufikia katika mashamba yao, waliharibu nyumba zao na kusema kuwa wanaondolewa hapo ili kutoa fursa kwa Grace Mugabe ya kujenga bustani ya michezo.
Baadhi ya familia
hizo zimenukuliwa zikilalamika kwamba, wameamriwa kuondoka katika makazi yao
hayo hata hivyo bila ya serikali kuwapatia eneo jingine la kuishi.
Wakati huo huo Taasisi ya Mawakili wa Haki za
Binadamu ya Zimbabwe imetuma timu ya wanasheria huko Mazowe ili kusitisha zoezi
la kuzifukuza familia zilizokuwa zikiishi hapo.