Wakati kampeni za uchaguzi mkuu zinaendelea, wagombea wameendelea
kutoa ahadi zinazolenga moja kwa moja matakwa ya wananchi katika maeneo
mbalimbali ambapo jana mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa
aliwagusa wakazi wa Morogoro.
Lowassa aliwaahidi wakazi hao kuwa akichaguliwa kuwa rais
atahakikisha anafuatalia na kutafakari taratibu na sheria kuona
uwezekano wa kukirudisha kiwanda cha sukari cha Mtibwa mikononi mwa
wananchi hao.
“Lakini ninaamini hilo suala linawezekana, kukitaifisha kiwanda hiki kuwa kiwanda cha umma,” alisema.
Katika hatua nyingine, Lowassa aliwaahidi wananchi hao kuwa
atahakikisha serikali yake inakuwa serikali rafiki ya wananchi wa kima
cha chini hususan mama ntilie, bodaboda na wafanyakazi wadogowadogo huku
akiisisitiza ahadi yake ya kuanzisha benki yao.
Kadhalika, Lowassa alisema kuwa ahadi ya serikali yake kuwa itatoa
elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu itazingatia utoaji wa
elimu bora na sio bora elimu.
No comments:
Post a Comment