Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kuondolewa vikwazo ni sehemu ya
mazungumzo ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa
ya wafanyaziara na majirani wa haram tukufu ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (as)
mjini Mash'had ambapo sambamba na kuashiria mazungumzo ya nyuklia ya Iran .
na
nchi za Ulaya na Marekani amebainisha kuwa, upande wa pili unaofanya mazungumzo
na Iran hususan Marekani una haja na mazungumzo na kwamba, hitilafu zilizoko
baina ya Wamarekani hazina maana kwamba, Washington haina haja na mazungumzo
haya.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, salamu za Rais
Barack Obama wa Marekani kwa mnasaba wa sikukuu ya Nouruz hazikuwa na ukweli na
kubainisha kwamba, Marekani ndiyo sababu kuu ya mashinikizo dhidi ya taifa la
Iran na imekuwa ikifanya kila iwezalo ili kulitwisha taifa hili ubeberu wake.
Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, hakuna mtu ndani ya Iran ambaye hataki kadhia
ya nyuklia ipatiwe ufumbuzi, bali kile ambacho taifa la Iran halikitaki ni
utumiaji mabavu, ubeberu na utwishaji mambo wa Marekani.
Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, taifa la Iran halitishwi na vikwazo wala
nguvu za kijeshi kwani limesimama kidete na liko imara.
Amebainisha kwamba,
katika mazungumzo yake na kundi la 5+1, Iran haifanyi mazungumzo kuhusiana na
masuala yasiyo ya kimantiki.
Aidha Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu
amesema, inachotaka Iran ni utulivu na kushikwa hatamu na wananchi wenyewe wa
mataifa ya Mashariki ya Kati, lakini siasa za Marekani ni kuleta vurugu na
machafuko.
http://kiswahili.irib.ir/habari/kiongozi/item/47526-iran-haitishwi-na-vikwazo-wala-nguvu-za-kijeshi