Askari mkoani Morogoro akiwa chini baada ya kupigwa na Wananchi wenye asirakali |
Askari
mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana
kwa jina la Ramadhani, ameuawa mchana huu na wananchi wenye hasira mjini
Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye
aliparamia lori.
Tukio hilo
linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa
wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi.
Mashuhuda
wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye
alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali
hiyo na kuanza kuwashambulia.
Baada ya
kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi
waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo kumwua polisi mmoja.
No comments:
Post a Comment