Saturday, April 25, 2015

Saudia yaogopa kivuli chake, ina woga itashambuliwa

Duru za usalama nchini Saudi Arabia zimetangaza hali ya tahadhari kufuatia ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo juu ya kuwepo uwezekano wa kushambuliwa vikali na upande ambao haikuutaja. 


Mansour Turki, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia amesisitiza kuwa, maeneo ya biashara, masoko na mshirika ya mafuta nchini humo hivi sasa yanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa wakati wowote ule.

 Amesema kuwa, hivi sasa polisi ya nchi hiyo inapitia kipindi kigumu mno katika kusimamia usalama ingawa hata hivyo hakutoa maelezo kamili juu ya suala hilo. 

Hii ni katika hali ambayo polisi ya Saudi Arabia imeanzisha operesheni ya kupekuwa magari katika maeneo ya mji mkuu Riyadh, bali hata watu wanaokwenda kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu al-Kaabah. 

Mwanzoni mwa wiki hii Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia, alitangaza kuwepo uwezekano wa nchi hiyo kushambuliwa na Harakati ya Answarullah ya nchini Yemen kufuatia mashambulizi ya kichokozi yanayoendelea kufanywa na Saudia dhidi ya nchi hiyo jirani ya Kiarabu.

No comments: