Kwa kweli Tunapenda Kumshukuru Mh. Raisi John Pombe Magufuli
kwa kusimama Kidete na Kupambana
kuhakikisha kwamba mpaka leo Ugonjwa huu bado unadhibitiwa kwa hali ya
Juu na kwa kiasi Kikubwa, yote hayo ni kwa juhudi ya Mh. Raisin a Serikali
yake.
Sisi kama Viongozi wa Dini ya Kiislamu na kama Wafuasi wa
Dhehebu ya Ahalulbayt (Shia
Ithnasheriya) tunapenda Kumshukuru Mhe. Raisi na Serikali yake kwa Kazi nzuri kama
ambavyo vile vile kwa mnasaba huu wa Israa na Miiraj na Kutumwa Mtume Muhammad
(s.a.w.w).
tunapenda Vile vile Kumshukuru Mufti wa Tanzania Sheikh
Abubakar Zuberi kwa Maelekezo yake makubwa na maelekezo yake mazito yanayoonyesha
Uweledi , yanayoonyesha Utaifa yanayoonyesha ni Mtu anaeitakia kheri Tanzania
hii iwe ya amani, iwe Tanzania isiyokuwa na Balaa la Ugonjwa wa Corona wala
aina zote za Maradhi, Tunapenda Kumshukuru kwa Maelekezo yake yote ambayo
ameyatoa namna ya Kupambana na janga hili la Coron.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwa Baraka la tukio hili la
Israa na Miiraj na Kupelekwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ninamuomba Mwenyezi Mungu
balaa hili la Corona tatizo hili la Corona Mwenyezi Mungu alisambaratishe ,
Watanzania wabakie Salama kwa balaa hili la Corona, Mwenyezi Mungu iangalie
Tanzania kwa Macho yako mawili ambayo hayalali, kama ulivyoiangalia inchi hii ukaifanya
ni nchi ya amani na Utulivu Mungu iangalie Vilevile uiepushie na balaa hili la
Corona. Israa, Miiraji na Biidha njema kwa Waislamu wote na kwa Watanzania
wote. Asanteni Sana na Mungu awabariki.
Na: Maulana Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya
Jumapili 22,03.2020, Dar es salaam.