Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umekiri
kwamba umetumia mabomu yaliyopigwa marufuku ya vishada katika
mashambulizi yake dhidi ya wananchi wa Yemen.
Ahmed al-Asiri, msemaji wa vikosi vya Saudia nchini Yemen
amesema ni kweli muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh dhidi
ya Yemen umetumia mabomu ya vishada yaliyotengenezewa Uingereza aina
ya BL755.
Amesema utawala huo umeamua kutotumia tena mabomu hayo ya vishada
katika hujuma zake nchini Yemen na kwamba watawala wa Riyadh
wameitaarifu Uingereza kuhusu uamuzi huo.
Mapema mwezi huu, Abdulaziz bin Habtoor, Waziri Mkuu wa Uingereza
aliituhumu Uingereza kuwa inafanya jinai za kivita nchini Yemen kwa
kuiuzia Saudia mabomu ya vishada.
Hivi karibuni Steve Goose, Mkurugenzi wa Kitengo cha Silaha cha
shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch aliitaka
Marekani kusimamisha uzalishaji na uuzaji wa mabomu ya vishada kinyume
na sheria za kimataifa kwa Saudia, huku akiutaka utawala wa Aal-Saud
kukoma kutumia mabomu hayo haramu dhidi ya raia wasio na hatia nchini
Yemen.
Watu zaidi ya 11,000 wameuwa katika hujuma za muungano vamizi wa
kijeshi unaoongozwa na Saudia nchini Yemen, mbali na kuharibiwa asilimia
kubwa ya miundomsingi, tangu Machi mwaka jana 2015.
No comments:
Post a Comment