Friday, July 1, 2016

"Tujitokeze kwa wingi kupinga dhulma wanayofanyiwa Wapalestina"Sheikh Jalala

Kiongozi Mkuu wa Waislamu Dhehebu la Shia ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akielezea jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Quds.
NICE MUSHI akiwaeleza waandishi wa habari alichoshuhudia huko Palestina, Munishi  amesema wakazi wa taifa hilo hususan Wakinamama watoto wanapata tabu sana, ambapo mtoto analzimika kutembea kilometa 13 za kufuata shule, hiinikulingana na ukuta Israel wameojenga.


Kiongozi wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania alisema Unapoiangalia historia ya wapalestina na yanayojiri katika ardhi ya watu hao sasa ni dhulma, unyonyaji na ukandamizaji ambao ni makosa ambayo hayatakiwi kunyamaziwa, kwakuwa hakuna shaka wala wasiwasi kuwa palestina ni ya wapalestina.

 Waislam, Wakristo na Wapenda amani nchini Tanania wataungana na Wapalestina wenzao na watu mbalimbali kote Duniani kuhadhimisha siku ya Quids Ijumaa Julai mosi ambapo watakuwa na matembezi yatakayoanzia Ilala Boma hadi viwanja vya Pipo Kigogo. alisema jana wakati akiongea na waandishi wa habari, katika ukumbi wa habari maelezo jijini dar es salaam na

Sheikh Jalala alisema wanayo yapata wapalestina ni matatizo makubwa na kwamba leo hii sio ajabu kuvunjiwa nyumba zao za ibada, Mwanamke kujifungulia kwenye vizuizi njiani na kubwa zaidi ni kushambuliwa na kuuliwa na wa Israel bila hatia.

Sheikh Jalala alieleza imani yake kwamba ili dunia iwe ana amani na mahala salama pa kuishi ni lazima kuitetea na kuunga mkono mapambano dhidi ya unyanyasaji, dhulma na uonevu dhidi ya wapalestina kwa alivyofanya Hayati Mwalimu Nyerere na Nelson Mandela kwa kile alichodai kuwa leo yapo Palestina ila kesho huenda yakaenea ulimwengu mzima katika dhana ya dini.

Quids ni siku ya Wapalestina na ukombozi wa mwanadamu Duniani kutoka katika uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji wa mwanadamu. Malengo yake makuu ni kuhamasisha amani katika nchi hiyo na kuwasaidia wapalestina wapate ukombozi.