|
Wapinzani wa ndoa za jinsia moja wakiandamana mbele ya mahakama kuu
Hukumu hiyo iliyopitishwa na majaji watano dhidi ya wanne imesema
uhakikisho wa katiba wa ulinzi sawa chini ya sheria unamaanisha kuwa
majimbo hayawezi kupiga marufuku ndoa za jinsia moja. Kufuatia hukumu
hiyo, ndoa za jinsia moja zitakuwa halali katika majimbo yote 50 ya
Marekani.
Jaji Anthony Kennedy, akiandika kwa niaba ya mahakama, amesema matumaini
ya wapenzi wa jinsia moja wanaopanga kuoana ni kutengwa na kuishi
maisha ya upweke, na kutenganishwa na taasisi za moja ya demokrasia za
muda mrefu zaidi duniani. "Wanaomba heshima sawa mbele ya sheria. Katiba
inawapa haki hiyo," amesema.
Kennedy ambaye hutoa kura ya maamuzi katika kesi katika kesi zenye mvuto
mkubwa, aliungwa mkono na wengine wa majaji wanne waliberali wa mahaka
hiyo. Kennedy ambaye aliteuliwa na rais Mrepublican Ronald Reagan mwaka
1988, hivi sasa ameandika hukumu zote muhimu nne kuhusu haki za mashoga,
ambapo ya kwanza ilikuja mwaka 1996.
"Bila kutambuliwa, utulivu na kutabirika kwa ndoa, watoto wao watateseka
na unyanyapa wa kujua kuw afamilia zao haziko sawa na nyingine,"
aliandika Kennedy. Katika maoni yanayokinzana, jaji mhafidhina Antonin
Scalia, alisema uamuzi huo unaonyesha kuwa mahakama hiyo ni tishio kwa
Wamarekani.
Jaji mkuu wa Marekani, mhafidhina John Roberts, alisoma muhtasari wa
upinzani wake kutokea nje ya chemba la majaji, hii ikiwa mara ya kwanza
kwake kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 10 aliokaa katika mahakama
hiyo. Roberts alisema ingawa zipo hoja za nguvu kisera katika suala la
ndoa za jinsia moja, halikuw ajukumu la mahakama hiyo kuyalaazimisha
majimbo kubadili sheria zake za ndoa.
| |
Obama, Clinton washerehekea, Republican walaani
Rais Barack Obama, ambaye ni rais wa kwanza alieko madarakani kuunga
mkono waziwazi ndoa za jinsia moja, alisifu hukumu hiyo, akisema kwenye
mtandao wake wa twitter kuwa siku ya leo ni hatua muhimu katika safari
ya kuhakikisha usawa kwa watu wote.
Naye Hillary Clinton, mgombea anaepewa nafasi kubwa kupitishwa na chama
Demokratic kuwania urais mwaka 2016, aliandika kwenye mtandao wake wa
twitter kuwa "Najivunia kusherehekea ushindi wa usawa wa ndoa." Hadi
mwaka 2013, Clinton alisema alikuwa anapinga ndoa za jinsia moja, lakini
alibadili mtazamamo wake tangu wakati huo.
Rais Barack Obama ameitaja hukumu hiyo kuwa ni ushindi wa usawa nchini Marekani.
Mgombea wa chama cha Republican Mike Hackabee alisema, uamuzi huu wa
udanganyifu ni uababe wa mahakama unaokwenda kinyume na katiba." Mgombea
mwingine wa Republican Jeb Bush aliongeza kuwa, " nikiongozwa na imani
yangum naamini katika ndoa za asili. Naamini mahakama kuu ilipaswa
kuyaruhusu majimbo yafanye uamuzi huu.
Ndoa za jinsia moja zilikuwa zinaruhusiwa katika majimbo 36 ya Marekani
pamja na Washington DC. Katika jimbo la 37 la Alabama, mahakama iliondoa
marufuku dhidi ya ndoa za jinsia moja, lakini mahakama ya rufaa
iliwazuwia maafisa wa serikali kutoa leseni kwa wapenzi wa jinsia moja.
Wapinzani wa ndoa hizo wanasema uhalali wake unapaswa kuamuliwa na
majimbo yenyewe, na wengine wanasema kuruhusiwa kwa ndoa hizo ni dharau
kwa ndoa ya asili kati ya mwanamume na mwanamke, na kwamba Biblia
inalaani mahusiano ya jinsia moja.
Hisia juu ya hilo zilikuwa juu wakati wa mjadala mahakamani mwezi April
katika kesi hiyo, pale mwandamanaji alipowapigia kelele majaji na
kuwambia wataozea jahanam ikiwa watapitisha hukumu kuunga mkono ndoa za
jinsia moja.Chanzo BBC Swahili