Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Duniani,
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ameongoza Swala ya maiti ya marehemu
Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani, rais wa zamani wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran.
Umati mkubwa ukiongozwa na viongozi wa ngazi za juu wa serikali
na wanazuoni wameshiriki Swala hiyo, iliyoswaliwa katika Chuo Kikuu cha
Tehran.
Takriban viongozi wote wa ngazi za juu wa Iran akiwemo Rais Hassan
Rouhani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Ali
Larijani na Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Ayatullah Sadeq Amoli Larijani.
Shughuli ya kusindikiza mwili wa marehemu Ayatullah Rafsanjani
inaanza saa nne asubuhi ikiongozwa na Rais Hassan Rouhani, mawaziri wa
serikali na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi wakifuatiwa na wananchi
katika Husainiya ya Jamaran. Mwili wa marehemu Ayatullah Rafsanjani
utazikwa kandokando ya kaburi la mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam
Ruhullah Khomeini katika eneo al Behest Zahraa katika viunga vya mjini
Tehran.
Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani aliyekuwa Mkuu wa Halmashauri ya
Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran alifariki dunia Jumapili
usiku kutokana na matatizo ya moyo
No comments:
Post a Comment