Mkuu wa dini ya Wayahudi nchini Israel, Chief Rabbi Yitzhak Yosef ambaye, wakati wa mahubiri aliwafananisha Waafrika na kima. |
KAMATI YA MSHIKAMANO WA TANZANIA NA PALESTINA
Dar
es Salaam
Risala
kwa Vyombo vya Habari
Israel ni nchi ya Ukaburu inayodhalilisha Waafrika
KAMATI ya Mshikamano wa
Tanzania na Palestina inalaani vikali matusi yaliyotamkwa na mkuu wa dini ya
Wayahudi nchini Israel, Chief Rabbi Yitzhak Yosef ambaye, wakati wa
mahubiri aliwafananisha Waafrika na kima.
Yosef ni mmoja kati ya
wachungaji wawili wakuu wanaoteuliwa na serikali ya Israel. Alipokuwa akihubiri
katika hekalu la Kiyahudi hivi majuzi aliwazungumzia Waafrika na akatumia neno
“kushi” amabalo katika lugha ya Kiibrania ina maana ya “kima” .
Hii si mara ya kwanza
kwa mchungaji huyu mkuu wa Israel kutumia maneno ya kuwadhalilisha Waafrika.
Katika mahubiri yake ya Mei mwaka jana alisema wanawake wana tabia ya wanyama
kwa sababu ya mavazi yao. Halafu mnamo Machi 2016 alitangaza kuwa watu wasio
Wayahudi hawapaswi kuishi nchini Israeli
Mawazo ya mchungaji
huyu hayakubaliki, lakini hayashangazi sana kwa sababu wakati wote Israel
yenyewe imekuwa na msimamo wa kuwabagua na kuwadhalilisha Waafrika na wazawa
Wakipalestina. Ukaburu huu umekuwa ukiongezeka, siyo tu miongoni mwa Wayahudi
wa Israeli bali hata miongoni mwa serikali ya Israel na watendaji wake.
Ndio maana hivi sasa
Israel iko mbioni kuwafukuza maelfu ya Waafrika wanaoishi na kufanya kazi huko.
Tayari onyo limetolewa kuwa kuanzia tarehe 1 Aprili 2018 kama Waafrika hao
hawataondoka basi watakamatwa na kufungwa gerezani bila kikom.
Israel imetangaza kuwa
Waafrika wanaoishi ni tishio kwa utambulisho wa Kiyahudi. Waziri mkuu wa Israel
Benjamin Netanyau amekuwa akitaka wafukuzwe na kusema kuwepo kwao nchini Israel
ni tishio kwa “amani na usalama”. Amesema Waafrika hao ni magaidi
Naye waziri wake wa
mambo ya ndani, Eli Yishai amesema Waafrika walio Israel wanapaswa wajue kuwa
nchi “hii ni yetu sisi watu weupe”. Na waziri wa utamaduni na michezo , Miri
Regev amesema Waafrika ni sawa na maradhi ya “saratani”
Hii ni Israel, nchi ya
kikaburu ambako wanafunzi katika chuo cha uhandisi wanaulizwa suali kuhusu
mapanya wanaopaswa kukamatwa na kuangamizwa. Mapanya hao si wengine bali ni
Waafrika
Hii imefanyika katika
chuo kikuu cha Ben-Gurion ambako mkuu wa kitivo cha uhandisi, “Profesa” Moshe
Kaspi ametoa suali kwa wanafunzi wake likisema katika kazi ya kuchimba mtaro
ili kujenga reli ya chini ya ardhi jijini Tel Aviv, wanakutana na mapanya
wengi. Inaamuliwa kuwasafirisha panya hao hadi Afrika ambako wanahitajika
katika utengenezaji ya chanjo ya kichaa cha mbwa.
Na ndio maana duniani
kote kumekuwepo na kampeni ya kulaani ukaburu huu wa Israel katika mtandao wa
jamii (#IsraeliApartheidWeek). Huko
Afrika Kusini kampeni hii iliendeshwa kati ya tarehe 12 na 18 Machi pamoja na
mikutano katika miji kadha. ili kupata habari kamili kuhusu huu ubaguzi na
ukaburu wa Israel dhidi ya Waafrika
Hata katika jiji la Tel
Aviv watu takriban 25,000 wamekusanyika kupinga sera ya Israel ya kuwafukuza
Waafrika ambao wameomba hifadhi.
Mabango yalibebwa
yakisema “Hakuna tofauti kati ya damu zetu, ni kwa sababu sisi sote ni
wanadamu”
Walikuwa wanapinga sera
ya Israel ya kuwasafirisha Waafrika hadi Rwanda na Uganda . Kati yao ni
watu karibu 38,000 kutoka Eritrea na Sudan ambao tayari wamepewa notisi yaa
kuondolewa na kupelekwa Uganda na Rwanda.
Hata Waafrika
walioingia Israel kwa kudai wao ni Wayahudi nao wanakabiliwa na tishio la
kufukuzwa. Chini ya ukaburu wa Israel sasa wanaambiwa wao sio Wayahudi
Almuradi Israel si
tofauti na Afrika Kusini wakati wa utawala wa makaburu.
Ndio maana ulimwengu
leo unaendesha kampeni ya kuwawekea vikwazo kama ilivyofanyika wakati ule wa
makaburu wa Afrika Kuini (BDS)
Aidha, Kamati inaungana na jumuiya ya Kimataifa
katIka maadhimisho ya siku ya ARDHI YA PALESTINIA kwa kulaani uendeleaji wa
uporaji wa ardhi ya Wapalestina. Katika maandamano ya Amani ya kuadhimisha siku
ya ARDHI yaliofanyika huko Ukanda wa
Gaza Wapalestina 17 waliuliwa
Maandamano hayo yanaendelea huko Gaza na jumla ya
Wapalestina 30 wameuliwa na mamia kujeruhiwa na wanajeshi wa Israel wanaotumia
risasi za moto, vifaru na mabomu ya machozi.
Kati ya waliouawa ni mwanahabari
wa Kipalestina aliyevaa nguo zilizomtambulisha kuwa ni mwandishi. Waandishi
wengine watano wamejeruhiwa
Tunalaani kwa nguvu zote mauwaji hayo. Kamati
inasikitika kwa jumuiya za kimataifa
kukaa kimya licha ya mauaji haya ya waandamanaji wasio na silaha yanayoendelea
hadi leo.
Kamati inaiomba serekali na Jamii ya Watanzania
kuzidi kupaaza sauti zao katika kulaani na kupinga ukandamizwaji na mauwaji
wanaofanyiwa ndugu zetu wa Palestina na watawala wa Israel
Kamati inawaomba Watanzania wasikae kimya katika
suala hili na tukumbuke maneno yafuatayo ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Ikiwa
kweli tunataka kumuenzi tuyatekeleze maneno yake kwa vitendo.
"Hatujawahi
kusita katika kuunga mkono haki ya watu wa Palestina kuwa na ardhi yao. Kizazi
chetu kilikuwa ni kizazi cha harakati za kitaifa kwa ajili ya uhuru wa nchi
yetu na hivyo ndivyo tulivyokuwa. Lakini masaibu ya Wapalestina ni mabaya zaidi
na yasiyo halali, wanaporwa nchi yao, wao ni taifa bila ardhi. Na kwa hivyo
wanastahili uungwaji mkono wa Tanzania na Dunia kwa ujumla."
-Mwalimu
Nyerere
AHSANTENI
ABDULLAH
M.OTHMAN
MWENYEKITI.
KAMATI YA
MSHIKAMANO WA TANZANIA NA PALESTINA