Saturday, May 2, 2015

Nafasi ya Dini katika kutangaza na kueneza Haki za Wanawake na Uadilifuk kwa jamii

Dkt. Riziki Ngwela, akitoa mada ya "Ushirikiano wa Madhehebu za Dini mbalimbali katika kuleta jamii ya Wanawake na KuzuiaUnyanyasaji dhidi ya Wanawake na Watoto.          Amesama kuwa Taasisi za Kidini zinapaswa kuhubiri maneno ya Mungu, kuelimisha na kusisitiza juu ya Ushirikiano na kutambuana. Aidha amesema kuwa zinapaswa kujenga Uadilifu katika jamii, ili kuleta amani na uongofu.
Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba yake katika semina iliyokusanya dini kuu mbili ya Uislamu na Ukristo katika kujadili "Nafasi ya Dini katika kutangaza na kueneza Haki za Wanawake na Uadilifu wa jamii", iliyoandaliwa na Ofisi ya Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Kiislamu wa Iran.       Sheikh Jalala amesema kuwa Imam ali (a.s) alisema Mwanadamu ametunukiwa Vitu muhimu Viwili, kati ya hivyo ni Amani, hiyo amewataka Watanzania kuienzi amani .Aidhaa amesema kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s), kama ni siku ya Amani, Upando , Ushirikiano, kuvumiliana.

Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA), Mama Shamim Khan, akitoa muongozo juu ya Watoa Mada, Pembeni yake ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, hapa Tanzania.

Mchungaji Rev, Thomas Father Goda akitoa mada yake inayosema "Nafasi ya Dini katika Kujanga na Kueneza Amani na Uadilifu wa Jamii kwa Wanawake"

Katikati ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislam wa Iran, akitoa shukrani na pembeni yake kulia ni Muakilishi wa Utamaduni wa Iran hapa Tanzania.

No comments: