Kiongozi Mkuu wa
Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala ametaka
Watanzania kuacha tofuati zao za Kidini, Kimadhehebu na Kimtazamo badala yake
wajikite kuwa kitu kimoja kwani ndio mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Kauli hiyo aliitoa
jana katika Matembezi ya Amani ya Kukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w),
matembezi amabayo yalianzia Makutano ya Morogoro Road na Kagera kuelekea Uwanja
wa Pipo Kigogo, Jijini Dar es salaam.
“Matembezi haya amani
mnayoyaona yaliyogubikwa na huzuni ya kumkumbuka Mtume Muhammad (s.a.w.w) iwe
ni chachu kwa waislamu wa Tanzania na waislamu wa Duniani kuacha tofauti
zao walizokuwanazo , tofauti zao za Madhehebu , tofauti zao za Kifikra, na kuwa
kitu kimoja kwasababu ndio usia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)” alisema Sheikh
Jalala
Sheikh Jalala alisema
kuwa Tanzania inahitaji Umoja wa Kitaifa ambao unasifa ya kuwaweka Watnzania
wote bila kujali Dini zao, Tofauti zao, Fikra zao, kwani wenyewe unazingatia
Ubinadamu kwanza.
“Kitabu hiki cha
Quran kimehimiza ni chambo la Umoja wa Ktaifa, Umoja wa uwanadamu, umoja wa
Watu, wanadamu wote wanahadhi moja, wanadamu wote ni kitu kimoja,dunia
inahitajia umoja wa Uwadamu, wanadamu kuwa kitu kimoja,inahitajia wasia wa
Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliouacha, wasia ambao unawataka watanzania wote
pamoja na dini zao tofauti na mitazamo yao tofauti, na mambo yao tofauti, na
ibada zao tofauti, lakini watambue wao wote ni kitu kimoja.”
Aidha Sheikh Jalala
alisema kuwa swala la Umuhimu wa Kukaa Vizuri na Watu wote, Kushirikiana, na
Umuhimu wa Amani ni miongoni mwa mafundisho cha Kitabu cha Quran na Wasia
alioucha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
“Kitabu hiki cha
Quran kinahimiza na kuenzi jambo la umuhimu wa Kukaa vizuri, umuhimu wa
Kupendana, umuhimu wa amani, Umuhimu wa mshikamano, umuhimu wa kuamini sisi
wote ni ndugu na sote ni watoto wa adamu, naamini yakwamba Tanzania inauhitajia
ujumbe huu.” Alisema Sheikh Jalala
Kwaupande wake Mmoja
wa Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya (T.I.C)
Taifa Mhe.Ramadhani Athumani Lisu amesema kuwa Watanzania wanahitaji malenzi na
Muongozo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Nyanja zote katika maisha ya kila
siku.
“Tanzania pamoja na
Dunia kwa ujumla inahitajia Malezi na Muongozo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)
katika nyanja zote kama Nyanja za elimu, Uchumi, Siasa, afya na Kilimo pamoja
na Mahusiano mema ya kiinchi.” Mh.Lisu alisema
Hatahivyo Mh. Lisu
alitoa wito kwa watanzania kuwa na imani pamoja na kuitenda kimatendo kuwa
Binadamu wote ni sawa na tunatakiwa kudhaminiana kama binadamu wote ni sawa.
"Wito wetu kwa
watanzania na Dunia kwa Ujumla kuwa wanadamu wote tudhaminiane, na tuzingatie
mafunzo na maelekezo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambayo inakwnda pamoja na
umuhimu wa Amani kwa watu wote."