|
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiwahutubia waumini wa Dini ya Kiislam |
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam katika kipindi hiki
cha uandikishaji wa daftari la kupigia kura, waumini wajitokeza kwa wingi kujiandikisha
ili kuja kuitumia haki yao ya msingi ya kumchagu mtu wamtakae.
“Kipindi hiki kinahitajia lugha za busara,na
maelewano,ni wajibu wa waislaam kisheria kujiandikisha na kupiga kura, “ni wajibu
wako wa kuwachagua Raisi, Mbunge na Diwani watakao leta maelewanao, Mshikamano,
Utulivu na Amani”amesema Jalala.
Ameyasema hayo katika swala ya ijumaa leo masjid
Ghadiir-Kigogo Post –ar es salaam, na kusema kuwa kitendo cha kumwita
mwenzako kua ni kafiri ni kusema kua damu Yake ni halali kumwagwa,na mali yake
ni halali, nahii ni hatari jamii kuitana majina mabaya, majina ambayo
yatasababisha damu ya mwenzio kumwagwa, na kumuhukumu kuingia motoni.
“kuitana majina
mabaya ni kuigawa jamii, na hakuna sababu ya kuitana majina mabaya wakati
waislaam wote wanasema Laailaha Illa Allah, Muhammada Rasuulu llah,”kitendo
cha mtu kumkiri mungu na mtume wake ni Heshima kubwa “ amesema Sheikh Jalala
Aidha Sheikh Jalala amewataka waislaam na watanzania
kwa ujumla kuwa kwayale yanayotendeka katika nchi za kiislaam, na Afrika za
kuhatarisha amani kwa kujiripua na Kukufurishana na mtu anaejita muislaam kua huo si uislaam na
wala uislaam hauelekezi hayo,
“Mwenye jina
zuri la kiislaam kuingia katika msikiti na kujiripua na kuwaua waislaam Na
Wakristo pamoja na watu wasiokuwa na hatia au kukamatwa mateka kwa wanawake na
kuuzwa sokoni, ni uislaam upi unaoruhusu wanawake kuuzwa? Tunasoma katika vita
ya jamali, uhudi, hivi ni vita gani wanawake waliuzwa? Uislaam gani
wanaouonyesha hawa? Aliuliza Sheikh Jalala.
Sheikh Jalala amewausia waumini kuuusoma uislaam halisi wa mtume Muhammad
(s.a.w.w) na kuuhubiri kwa watu, na kuachana na huu uislaam wa chinja chinja na
wa kuleta fakra kwa watu na jamii,
Hatahivyo Sheikh Jalala alihoji kuwa hivi hiki
kibali cha kuwaingiza watu motoni wamekitoa wapi? Ni mwenendo wa mtume kweli
hata wale wasio waislaam kuwaita makafiri? Laa hapana bali mtume (s.a.w.w)
alikua akiwaita kwa majina mazuri, ndio maana hata katika mjadala na wakristo
wa Najran, mungu aliwaita ya Ahlal kitab, iweje mwislaam mwenzio umuite kafiri?