Saturday, July 25, 2015

Ni wajibu kwa Mwislam Kujiandikisha Kupiga Kura-Sheikh Jalala.

Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiwahutubia waumini wa Dini ya Kiislam
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam katika kipindi hiki cha uandikishaji wa daftari la kupigia kura, waumini wajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuja kuitumia haki yao ya msingi ya kumchagu mtu wamtakae.
“Kipindi hiki kinahitajia lugha za busara,na maelewano,ni wajibu wa waislaam kisheria kujiandikisha na kupiga kura, “ni wajibu wako wa kuwachagua Raisi, Mbunge na Diwani watakao leta maelewanao, Mshikamano, Utulivu na Amani”amesema Jalala.
Ameyasema hayo katika swala ya ijumaa leo masjid Ghadiir-Kigogo Post –ar es salaam, na kusema kuwa kitendo cha kumwita mwenzako kua ni kafiri ni kusema kua damu Yake ni halali kumwagwa,na mali yake ni halali, nahii ni hatari jamii kuitana majina mabaya, majina ambayo yatasababisha damu ya mwenzio kumwagwa, na kumuhukumu kuingia motoni.

 “kuitana majina mabaya ni kuigawa jamii, na hakuna sababu ya kuitana majina mabaya wakati waislaam wote wanasema Laailaha Illa Allah, Muhammada Rasuulu llah,”kitendo cha mtu kumkiri mungu na mtume wake ni Heshima kubwa “ amesema Sheikh Jalala
Aidha Sheikh Jalala amewataka waislaam na watanzania kwa ujumla kuwa kwayale yanayotendeka katika nchi za kiislaam, na Afrika za kuhatarisha amani kwa kujiripua na Kukufurishana na  mtu anaejita muislaam kua huo si uislaam na wala uislaam hauelekezi hayo,

 “Mwenye jina zuri la kiislaam kuingia katika msikiti na kujiripua na kuwaua waislaam Na Wakristo pamoja na watu wasiokuwa na hatia au kukamatwa mateka kwa wanawake na kuuzwa sokoni, ni uislaam upi unaoruhusu wanawake kuuzwa? Tunasoma katika vita ya jamali, uhudi, hivi ni vita gani wanawake waliuzwa? Uislaam gani wanaouonyesha hawa? Aliuliza Sheikh Jalala.

Sheikh Jalala amewausia waumini kuuusoma uislaam halisi wa mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuuhubiri kwa watu, na kuachana na huu uislaam wa chinja chinja na wa kuleta fakra kwa watu na jamii,
Hatahivyo Sheikh Jalala alihoji kuwa hivi hiki kibali cha kuwaingiza watu motoni wamekitoa wapi? Ni mwenendo wa mtume kweli hata wale wasio waislaam kuwaita makafiri? Laa hapana bali mtume (s.a.w.w) alikua akiwaita kwa majina mazuri, ndio maana hata katika mjadala na wakristo wa Najran, mungu aliwaita ya Ahlal kitab, iweje mwislaam mwenzio umuite kafiri?

No comments: